Pichani ni mafundi wakiendelea kumalizia ujenzi wa chumba hicho.
Sayansi
ya Teknolojia ikiwa inaendelea kushika kasi siku hadi siku, chumba hiki
maalum kilichojengwa juu ya safu za milima ya Alpine iliyopo Ufaransa
kimepata kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wanaotokea sehemu mbalimbali
Duniani kutokana na staili ya aina yake walivyokitengeneza kwa kutumia
vioo vilivyozunguka kichumba hicho kidogo hivyo kumuwezesha mtalii
kuona kama vile yupo juu ya Dunia.
Unaambiwa
sio rahisi kwa mtu mwenye roho nyepesi kuweza kusimama kwenye kichumba
hicho kidogo kutokana na kuwa kileleni mwa mlima Alpine takribani
umbali wa mita 3800 kutoka usawa wa bahari ambapo utengenezaji wake
ulichukua takribani muda wa miaka miwili na ada ya kutembelea kwenye
kivutio hicho ni kiasi cha Euro 55 ambazo ni sawa na Tsh 80,000 bila
chenji.
0 comments:
Post a Comment