Leo usiku Arsenal wanatinga Uwanjani kwao Emirates kurudiana na Klabu ya
Uturuki Besiktas kwenye Mechi ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo yaLigi mabingwa barani Ulaya.
Wiki iliyopita huko Instanbul, Besiktas na Arsenal zilitoka 0-0 na
Arsenal wanahitaji ushindi tu ili kufuzu kwani Sare yeyote ya Magoli
itamaanisha Besiktas ndio wataingia hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ambayo droo yake itafanyika huko Monaco Siku ya Alhamisi.
Arsenal wanaingia kwenye Mechi hii bila ya Kiungo wao mahiri Aaron
Ramsey ambae alipewa kadi nyekundu kwenye Mechi ya Kwanza huko
Instanbul.
Pia Arsenal itamkosa Nahodha wao Mikel Arteta mwenye tatizo la Enka
na vile vile kumkosa Straika wao Olivier Giroud ambae pia ameumia Enka.
Kukosekana kwa Giroud kunaweza kutoa namba kwa Chipukizi Yaya Sanogo
au Lukas Podolski au hata Alexis Sanchez kuchezeshwa kama mshambuliaji au
ikibidi, Arsene Wenger kumtumia Joel Campbell.
Wakati Besiktas wana Kikosi kamili na Straika wao Demba Ba yu tayari
kurejea tena Jijini London kuitesa Arsenal kama alivyokuwa akifanya
akiwa na Klabu yake ya zamani Chelsea, Klabu hiyo ya Uturuki itakuwa
bila ya Meneja wao kutoka Croatia kwenye Benchi, Slaven Bilić, ambae
alipewa Kadi Nyekundu katika Mechi ya Kwanza na hivyo kulazimika kukaa
Jukwaani kwa Mechi hii.
0 comments:
Post a Comment