Facebook

Sunday, 24 August 2014

Maiti iliyozikwa miaka 700 iliyopita yapatikana haijaoza.


Maiti hiyo ikiwa imetolewa nje ya jeneza 
Ama kweli ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni....Maiti ya mwanamke iliyozikwa miaka 700 iliyopita yagunduliwa China ikiwa haijaoza. Ipo katika hali nzuri kiasi kwamba bado ina nyusi. Inasemekana alihifadhiwa vizuri na inaonyesha alikuwa ni mtu kutoka katika familia ya ufalme.

Maiti hiyo iligunduliwa na wafanyakazi wa barabara (wakandarasi) huko China mashariki walipopewa kaziya kupanua barabara katika mji wa Taizhou, Mkoani wa Jiangsu. Wakandarasi hao walitakiwa kuchimba kwenda chini kiasi cha futi 6 ili kumaliza mwinuko uliokuwa katikati ya bara bara ndipo wakakutana kitu wasichotarajia kukikuta.

Walipokuwa wakichimba walikuta kitu kigumu na baada ya kufanya utafiti wao kidogo ndipo waligundua kuwa kulikuwa kuna kaburi alilozikwa mtu na ndipo wakawaita wataalamu ili kuchunguza zaidi, baada ya hapo wakaamua kuweka wazi juu ya tukio hilo kuwa waligundua kwamba kaburi hilo lilikuwa na umri wa miaka 700. Tazama picha zaidi la sakata hilo hapa chini... 
 
Mkandarasi akijaribu kuvunja zege lililozunguka sanduku lakini kabla hawajajua kuwa kuna maiti! 
Baada ya kuvunja sanduku hilo la zege 
Wakihamaki baada ya kuona kitu ndani ya sanduku 
Wakianza kufunua matambara yaliyo ndani ya sanduku yaliyozunguka maiti.


0 comments:

Post a Comment