Manchester United wamekubali kutoa pauni
milioni 59.7 kumsajili Angel Di Maria kutoka Real
Madrid, na kuvunja rekodi ya uhamisho ya
Uingereza.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 26,
yuko mjini Manchester na atafanya vipimo vya
afya siku ya Jumanne, kabla ya kukamilisha
uhamisho ambao, ukithibitishwa utafikisha pauni
milioni 132 zilizotolewa na Manchester United
msimu huu kusajili wachezaji.
Huenda Di Maria akacheza mechi yake ya kwanza
dhidi ya Burnley siku ya Jumamosi, mchezo wa
ligi kuu.
Ada hiyo itazidi rekodi ya uhamisho ya Uingereza
ya pauni milioni 50 zilizotolewa na Chelsea
kumchukua Fernando Torres kutoka Liverpool
mwaka 2011.
Manchester United mara ya mwisho walivunja
rekodi ya Uingereza ya uhamisho mwaka 2002
walipotoa pauni milioni 29.1 kumsajili Rio
Ferdinand kutoka Leeds United.
0 comments:
Post a Comment