Facebook

Thursday, 28 August 2014

"Wosia wa Kanal Muammar Gaddafi kabla ya kifo Chake"....Jicho langu la tatu kwa Muammar Gaddafi

 
Nilipokuwa nachukua masomo yangu ya kidato cha Tano na Sita katika shule ya sekondari St.Matthew's iliyoko maeneo ya Mbagala jijini Da Es Salaam.Nilibahatika kusoma na watu wenye upeo mkubwa katika masuala ya Siasa,kwa bahati nzuri nilikuwa nalala sehemu moja na viongozi wa Wanafunzi katika shule hiyo kwa wakati huo,Viongozi hao ambao ni Tician Mabele Marando na Bob Chacha Wangwe kwa kiasi fulani ni wakomavu katika masuala mbalimbali ya siasa zaidi yangu.Niliweza kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na siasa ya Nchi yetu na ya dunia kupitia wao.

Vilevile nilisoma na kijana mmoja mwenye itikadi ya kipekee sana,ukipata wasaa wa kuzungumza nae moja kwa moja utajua huyu mtu kuna kitu cha ziada katika kichwa chake,alikuwa ni mtu wa kuongea kwa misamiati migumu sana kiasi kwamba ukitaka kumuelewa ni lazima ufikirie mara mbili kile alichokisema.

Nakumbuka ilikuwa ni tarehe 20 Oktoba mwaka 2011 siku ambayo tulipata taarifa kuwa kiongozi shupavu,hodari na mweye msimamo Kanali Muammar Gadaffi wa Libya ameuawa na majeshi ya NATO huko Sirte-Libya.

Baada ya tukio hilo nilihaha sana kutaka kujua kiundani zaidi kuhusiana na tukio hilo lakini sikufanikiwa;kwa sababu sheria za shule zilitubana katika kumiliki vitu ambavyo vingetusaidia kupata taarifa na mawasiliano.

Marjan Murshid;mwanafunzi ambaye ni nikimuangalia kwa jicho la pili namuona kama alikuwa amebarikiwa kipaji kikubwa katika kuongea na kutafakari mambo kwa weledi.

St.Matthew's walikuwa na uataratibu uliokuwa unaitwa "MORNING SPEECH",Marjan Murshid alijitolea siku hiyo,na kikubwa alichokiongea ni kuhusiana na tukio lililotokea siku hiyo;Kifo cha Simba na shujaa wa Afrika aliyekuwa amesalia.

Aliongea kwa uchungu sana na kikubwa ninachokikumbuka katika "SPEECH" yake ni jinsi gani Nchi za kibepari zianaingilia uhuru wa nchi za Kiafrika kwa kutumia mabavu na vilevile alizungumzia ni jinsi gani viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika{AU} walivyomsaliti na kumuacha peke yake apambane na wavamizi wa kibepari waliokuwa wanatumia kimvuli cha Majeshi ya NATO.
  Niliguswa sana na "SPEECH" ya Marjan Murshid.
 

Baada ya vuguvugu za katika mpya katika nchi yetu,vitendo vya kigaidi vinavyoripotiwa katika sehemu mbalimbali nchini kama vile Milipuko ya mabomu ya kutegwa huko Arusha na Zanzibar,kumwagiwa tindikali kwa watu mbalimbali.Vilevile unyama unaofanywa na Boko Haram huko Nigeria kwa kuwateka wanafunzi katika shule Kaskazini mwa Nigeria na baadhi kuwaua,hivi sasa kumeripotiwa kuwa Boko Haram wanataka kujitenga na Nigeria,wanataka kutengeneza nchi yao katika majimbo wanayoyakalia ;jicho langu pia limeangazia Ubinafsi wa viongozi wetu,ulaji rushwa na ukiritimba uliokithiri vimenifanya nimkumbuke shujaa na Simba wa Afrika aliyesimama imara katika kuendelea ndoto za nyota zilizozimika zilizopigana na kupinga vikali ukoloni na matawi yake.
 
Viongozi kama Haile Selassie,Ahmed Sekou Toure,Kwame Nkurumah,W.E.B Du Bois,Malcom X,Martin Luther Jr,Marcus Garvey walikuwa na ndoto kubwa sana ya kuwaunganisha Watu weusi popote walipo na kuwa kitu kimoja,Kwake Nkurumah alisema "African Should Unite" .Du Bois.Pan Africanism  "Power consolidation in Africa".
 

JICHO LANGU LA TATU KWA KANAL MUAMMAR GADDAFI
Mnamo mwaka 1942 Simba na shujaa wa Afrika ,mtoto wa mkulima Mohammad Abdul Salam bin Hamed bin Mohammad,aliyefahamika kama Abu Miniar{Aliyefariki mwaka 1985} na mama yake Aisha{alifariki 1978} alizaliwa katika "kijumba kidogo" kijiji cha Sirte katika jangwa kaskazini mwa Libya,eneo lilikuwa linakaliwa na watu wa kabila la Qadhadhafa, hapo ndipo nyota iliibuka ikaitwa Colonel Muammar Gaddaffi.

Kipindi Gaddafi anakua alishuhudia mapambano makali ya Vita ya pili ya dunia kati ya Italia na Uingereza huko Libya. Na kipindi Waitaliano wanaivamia Libya mwaka 1911 walimuua a babu yake Abdessalam Bouminyar.

Alisomea elimu yake ya awali huko Sebha-Libya ambapo walimu wengi walikuwa ni Wamisri na mwalimu wake kipenzi alikuja kuwa  Rais wa Misri,Abdul Nasser na alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi hodari sana.

Baada ya kushuhudia vipindi na machafuko mbalimbali kama vile Vita kati ya Israel na Waarab mwaka 1948,Suez Crisis 1956,Mapinduzi ya Misri 1952 alivutiwa sana na kufanya mabadiliko katika taifa lake la Libya lilokuwa masikini na dhaifu wakati huo.

Gaddafi ambaye alikuwa sio maarufu sana akiwa kijana mdogo mnamo Oktoba mwaka 1961 alipinga waziwazi kufukuzwa kwa Syria katika umoja wa nchi za Kiarabu kwa kuandaa vipeperushi na kuvisambaza karibia sehemu kubwa ya Libya,hakuishia hapo alikwenda kuvunja kioo katika hoteli moja kwa sababu ya kuuza pombe katika eneo analoishi,Gaddafi akaanza kujulikana kwa watu mbalimbali kutokana na misimamo yake thabiti.

Baadae Gaddafi alihama yeye na familia yake wakaenda kuishi Misrata.Akajiunga na shule ya sekondari Misrata alikataa kujiunga katika vyama vilivyofungiwa wakati huo.
Alipendezwa sana na somo alilofundishwa na Abdul Nasser lililokuwa linahusiana na Mapinduzi yaliyofanyika Ufaransa,vilevile alivutiwa na historia ya Abraham Lincoln.

Mnamo mwaka 1963 alijiunga na Chuo Kikuu cha Libya huko Benghazi ambako alijiunga na Chuo cha mafunzo ya kijeshi "Royal Millitary Academy"
Gaddafi alikuwa mzaleendo kwelikweli alikataa kujifunza kiingereza kwani aliwaona Waingereza kama wanyonyaji katika nchi hiyo.N alihusika katika kifo cha kamanda wa Kiingereza mwaka 1963
Alipohitimu masomo yake 1965 alitengeneza kikundi cha kimapunduzi alichokiita "Free Officers Movement".
Serikali ya Libya kipindi hicho ilimdharau Gaddafi na kumuona kama mtu ambaye hana madhara,Lakini alizunguka nchi nzima akihamasisha vijana mbalimbali kuungana nae katika chama chake.

Mwaka 1966 alikwenda Uingereza kupata mafunzo ya kijasusi na kijeshi na akafanikiwa kujifunza kiingereza huko Beacaconsfield,Buckinghamshire

Aliporejea Libya alianzisha vuguvugu nchi nzima baada ya wimbi la rushwa,Utumiaji mbaya wa rasilimali za nchi hasa mafuta na King Idris aliyekuwa kiongozi wakati huo..

Mwaka 1969 Idris alikwenda kupumzika Uturuki na Ugiriki na Gaddafi alichukua mwanya huo kufanya mapinduzi.Mnamo Septemba 1 Gaddafi na jeshi lake waliteka Viwanja vya ndege na vituo vyote vya polisi na radio.

Gaddafi aliandika kitabu chenye historia kubwa ambacho kilieleza malengo yale yote kuhusiana na yeye kuipundua serikali iliyokuwa madarakani "DE FACTO".

Asilimia 90 ya wakazi walimuelewa na kumpenda Gaddafi ambaye aliwahaidi maisha bora.
Alianzisha programu mbalimbali za kimaendelea ambazo baadae zilizaa matunda.Huku akitia mkazo zaidi katika uzalishaji wa mafuta na kuyauza kwa manufaa ya wananchi wa Libya.

Lakini baada ya uhasama baina yake na mataifa ya kibepari hususan kwa kitendo cha cha kuuza mafuta katika nchi za Masharaki ya kati na mashariki ya mbali.Nchi za kibepari ziliandaa njia nyingi za kumpindua lakini leo sitaelezea dhahiri shahiri sababu zilizopeleka kupindiliwa kwa utawala wa Kanali Mummara Gaddafi.Endelea kutembelea www.bantutz.com utapata kujua sababu za kupinduliwa kwa Gadafi.

Baada ya mapigano ya muda mrefu kati ya Majeshi ya Gaddafi na Majeshi ya waasi ambao kwa jicho langu la tatu ni kivuli cha mataifa ya kibepari kwani walikuwa wanasaidiwa na nchi za kibepari kwa mwamvuli wa majeshi ya kulinda amani ya NATO
 Image result for pictures of muammar gaddafi deathImage result for pictures of muammar gaddafi deathImage result for pictures of muammar gaddafi deathImage result for pictures of muammar gaddafi deathImage result for pictures of muammar gaddafi deathImage result for pictures of muammar gaddafi death
 Image result for pictures of muammar gaddafi deathImage result for pictures of muammar gaddafi deathImage result for pictures of muammar gaddafi death
Gaddafi Kabla ya kifo chake aliacha Ujumbe mzito ambao mtu yeyeto akiusoma atabubujikwa na machozi moyoni mwake.

Hapa chini nimekuandalia wosia alioucha Hayati,Simba wa Afrika,Kanali Muammar Gaddafi  kwa Waafrika na dunia nzima kiujumla.
Kwa kutambua kuwa wasomaji wa www.bantutz.com wapo wanaojua Kiingereza na wengine hawajui,nimetafsiri wosia huu kwa lugha mama ya Kiswahili (kisicho rasmi) lakini pia imeambatanishwa na iliyo katika lugha ya kiingereza.
 

-QADAFFI ANAANZA HIVI:

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah),Mungu mpaji, na mwenye rehema....Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba,hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi
nzuri ya kilimo.


Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani),alipomuua binti yangu niliyemuasili.
Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini.

Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU. Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.Lakini hawakuridhika.  


Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika.
Alihitaji zaidi. Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia"
na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni
mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo. Walikua hawasikii wala hawaoni.
Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure,elimu bure na chakula cha bure.(Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu). 


Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal
Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.
 

Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu.
Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.Ili achukue uhuru wetu, achukue haki
yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu.Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.
 

Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya.Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.
Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu,na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni.
 

Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.
Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu,nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache
waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye
himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na
imekuwa wazi kwa watu wangu.Nitapambana hadi pumzi yangu ya
mwisho ili watu wangu wawe huru.Mwenyezi Mungu atusaidie tubakiwaaminifu na tuwe huru.

             -- Mu'uammar Qaddafi.
          

(MAKALA YA KIINGEREZA)

GADDAFFI'S LAST SPEECH: In the name of Allah, the beneficent,the merciful...For 40 years, or was it longer, I can't remember, I did all I could to give people houses, hospitals, schools, and when they were hungry, I gave them
food. I even made Benghazi into farmland from the desert, I stood up to attacks from that cowboy Ronald Reagan, when he killed my adopted orphaned daughter, he was trying to kill me, instead he killed that poor innocent child. Then I helped my brothers and sisters from Africa with money for the African Union.I did all I could to help people Understand the concept of real democracy, where people's committees ran our country. But that was never enough, as some told me,even people who had 10 room homes,
new suits and furniture, were never satisfied, as selfish as they were they wanted more. They told Americans and other visitors, that they needed "democracy" and "freedom" never realizing it was a cut throat system,where the biggest dog eats the rest,but they were enchanted with those words, never realizing that in America, there was no free medicine,no free hospitals, no free housing, no free education and no free food,except when people had to beg or go
to long lines to get soup.No, no matter what I did, it was never enough for some, but for others, they knew I was the son of Gamal Abdel Nasser, the only true Arab and Muslim leader we've had since Salah-al-Deen, when he claimed the Suez Canal for his people, as I claimed Libya, for my people, it was his footsteps I tried to follow, to keep my people free from colonial domination - from thieves who would steal from us.Now, I am under attack by the biggest force in military history, my little African son, Obama wants to kill me, to take away the freedom of our country, to take away our free housing, our free medicine, our free education, our free food, and replace it with American style thievery, called
"capitalism" ,but all of us in the Third World know what that means, it means corporations run the countries, run the world, and the people suffer.So, there is no alternative for me, I
must make my stand, and if Allah wishes, I shall die by following His path, the path that has made our country rich with farmland, with food and health, and even allowed us to help our African and Arab brothers and sisters.I do not wish to die, but if it comes to that, to save this land, my people,all the thousands who are all my
children, then so be it.Let this testament be my voice to the world, that I stood up to crusader attacks of NATO, stood up to cruelty,
stood up to betrayal, stood up to the West and its colonialist ambitions,and that I stood with my African brothers, my true Arab and Muslim brothers, as a beacon of light.When others were building castles, I lived in a modest house, and in a tent. I never forgot my youth in Sirte,I did not spend our national treasury foolishly, and like Salah-al-Deen, our great Muslim leader, who rescued Jerusalem for Islam, I took little for myself... In the West, some have called me "mad", "crazy", but they know the truth yet continue to lie, they know that our land is independent and free, not in the colonial grip, that my vision, my path, is, and has been clear and for my people and that I will fight to my last breath to keep us
free, may Allah Almighty help us to remain faithful and free


ANGALIA HAPA VIDEO YA KIFO CHA GADDAFI

Nimeandaa makala hii kwa uchungu mkubwa sana ukifuatilia kwa umakini utagundua kubwa Gaddafi alikuwa ni muhimili mkubwa sana na mtu asiye na woga. 
   Ni kiongozi shujaa aliyeweza kupambana na Mabepari hadi dakika ya mwisho hakukubali kuongozwa aliamini Falsafa yake.
        Bara letu limebakiwa na Shujaa mmoja tu kiuhalisia,Robert Mugabe aliweza kuwapora Wazungu ardhi kubwa waliyokuwa wanaimiliki Zimbabwe na kuwapa Waafrika waliokuwa watumwa katika nchi yao wenyewe,ama hakika ni mafano wa kuigwa.

Nina amini rasilimali zilizopo katika nchi hii zinaweza kubadili historia yetu ya kuwa kichwa cha mwenda wazimu katika kila nyanja ya maisha;huduma duni za kiafya.Elimu mbovu inayozidi kudidimia na kukosa dira,miundombinu mibovu,ukosefu wa huduma nzuri za umeme.Ukiritimba unaoendelea katika mbuga za wanyama. 

       "MABADILIKO NI MIMI,NI WEWE,NI SISI"

 
Imeandaliwa na.................
                                              Katemi Methsela.
                                             {C.E,O BantuTz} 


Endelea kutembelea www.bantutz.com makala nzuri zaidi za kuvutia na kusisimua zinakuja.Tembelea site yetu uweze kuongeza ujuzi na maarifa.

0 comments:

Post a Comment