Lionel Messi alifunga mabao
mawili na kuisaidia Barcelona kuilaza Elche mabao 3-0 katika mechi
ya kwanza ya mkufunzi mpya Luis Enrique .
Barca wangesajili ushindi mkubwa zaidi ila tu mchezaji mpya Munir aligonga mwamba sawa na Andres Iniesta.Sekunde chache baadaye Javier Mascherano alitimuliwa uwanjani baada ya kumchezea visivyo Garry Rodrigues.
Barca ilienda mapumzikoni ikiwa kifua mbele na ilirejea ikiwa na hamu ya kutamatisha ushindi huo.
Mashambulizi yalianza moja kwa moja na Munir El Haddadi alifungia Barca bao la pili kunako dakika moja baada ya kipindi cha pili kuanza.
Kuanzia hapo haikuwa siri vijana wa Enrique walikuwa na niya ya kufungua ukurasa mpya msimu huu.
Kwa kocha Enrique ambaye alimrithi Tata Martino, ushindi huu ulikuwa dalili ya mambo kubadilika baada ya Tata kuiongoza Barcelona kwa msimu wake wa kwanza ambapo walikosa kushinda taji lolote tangu mwaka wa 2007-2008.
Enrique aliwasajili wachezaji wapya Luis Suarez kutoka Liverpool, Ivan Rakitic kutoka Sevilla na Thomas Vermaelen kutoka Arsenal ilikuimarisha nafasi zake za kutwaa ligi na hata kombe la mabingwa barani Ulaya.
Kocha huyo alikuwa hata na wasaa wa kuwashirikisha wachezaji wapya Rakitic, kipa Claudio Bravo, mlinzi Jeremy Mathieu washambulizi wachanga Munir na Rafinha ilikuwa na uhakika wa utendakazi wao uwanjani.
0 comments:
Post a Comment