Malaysia iko katika siku ya
maombolezi ya kitaifa baada ya kupokea miili 20 ya wahanga wa mkasa wa
ndege ya Malaysia MH17 iliyotunguliwa Ukraine mwezi uliopita.Miili ilipokelewa na kupewa heshima za kitaifa.
MH17 iliangushwa katika eneo la waasi Mashariki ya Ukraine mwezi uliopita.
Machi mwaka huu ndege nyingine ya Malaysia ilitoweka katika bahari hindi na shirika hilo la ndege linaendelea kutatizwa na matukio hayo mawili.
Ndege iliyobeba miili hiyo ilikuwa imetengwa kwa ajili ya shughuli hiyo kutoka Amsterdam na kutua saa nne saa za huko.
Bendera ya taifa itapepea nusu mlingoti kote nchini na dakika moja ya kimya itazingatiwa.
Kikundi kidogo cha wanajeshi wa Malaysia kilienda hadi karibu na ndege hiyo kulinda majeneza hayo yalipokuwa yakitolewa kwa ndege huku magari makubwa meupe ya mazishi yakiwa yamepangwa kuzipokea miili hiyo.
Majeneza yote yamefunikwa kwa bendera ya taifa na miili mitatu ya hiyo 20 imechomwa nchini Uholanzi.
Vibanda maalum kwenye barabara kuu vitakuwa na ishara za kielektroniki kuwaeleza madereva washuke kutoka kwa magari yao ilikutoa heshima.
Msemaji wa ndege za Malaysia alisema kwamba kampuni hiyo ingepanga kipindi cha maombi ambacho kingefanywa wazi kwa mtu yeyote ili kutoa maombi na heshima zao kwa walioaga.
Akiongeza alisema kwamba kampuni hiyo ya ndege za Malaysia imehuzunishwa sana na tukio hilo la kuogofya .
Aidha imekuwa muda mrefu wa kungoja kwa familia na marafiki wa wasafiri na wafanyakazi waliokuwa katika ndege MH17.
Heshima hiyo kitamaduni imekuwa ikipewa familia ya mfalme na wakuu serikalini.
Kufikia sasa waathiriwa 28 wa Malaysia wametambuliwa nchini Uholanzi ambako utafiti wa kimataifa kuhusiana na kuanguka kwa ndege hiyo mashariki mwa Ukraine unaendelezwa.
Zaidi ya majeneza 200 iliyo na mabaki ya waathiriwa kufikia sasa yamepelekwa Uholanzi lakini uchunguzi unazuiliwa na mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya serikali ya Ukraine na waasi yanayoiunga mkono Urusi karibu na eneo ambalo ndege hiyo ilianguka.
0 comments:
Post a Comment