Facebook

Thursday, 27 November 2014

Bi harusi wa miaka 14 ampa sumu mumewe

Bi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria
ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne
akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya
kuweka sumu ya panya katika chakula
alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake.

Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki
za kibinaadamu ambao wamesema kuwa
msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara
mbili umri wake anafaa kuchukuliwa kama
mwathiriwa na wala sio muhalifu.
Wasila tasiu kutoka familia masikini katika
eneo la waislamu la kazkazini huenda
akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa.

Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka
Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana
wa miaka 7 anayejulikana kama
hamziyya,ambaye alikuwa akiishi katika
nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe
Umar sani,wakati bi haru huyo alipoweka sumu
ya panya katika chakula hicho.
Hamziyya alijulikana tu kama dadaake mke wa
kwanza wa bwana Sani,mwanamke aliyeolewa
na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa
za wake wengi zimekithiri.

Msichana huyo wa miaka 7 alisema kwamba
Tasi'u alimpa fedha ili kununua sumu ya panya
kutoka duka moja jirani mnamo tarehe 5
mwezi Aprili,siku ambayo bwana Sani alifariki.
''Alisema kuwa panya wanamsumbua katika
chumba chake'',Hamziyya aliiambia
mahakama.Upande wa mashtaka baadaye
ulisema kuwa badala yake Tas'u aliweka sumu
hiyo ya panya katika chakula ambacho alikuwa
amekiandaa kwa sherehe za baada ya harusi
kwa kuwa alijuta uamuzi wake wa kumuoa
bwana Sani.

Msichana huyo alikataa kuzungumza
mahakamani.
Jaji Mohammed Yahaya,katika mahakama ya
Gezawa alitoa hukumu kwamba Tasi'u ambaye
alikataa kuongea katika mahakama hana hatia
katika kusikizwa kwa kesi mnamo mwezi
Octoba ambapo alisomewa mashtaka.
Jaji huyo alikataa ombi la upande wa
mshtakiwa la kesi hiyo kupelekwa katika
mahakama ya watoto.

Ushahidi wa Hamziyya uliungwa mkono na
Abuwa Yussuf muuzaji duka katika mji wa
Unguwar Yansoro ambaye alithibitisha kuuza
sumu hiyo kwa mtoto huyo.
Jirani ya Bwana Sani mwenye umri wa miaka
30 ambaye ni mkulima, Abdulrahim Ibrahim
alitoa ushahidi ambapo alisema kwamba
alipewa chakula hicho kilichopikwa na
Tasiu.''Nilipoletewa chakula hicho niliona
vipande vipande vyeusi''aliiambia mahakama.
Alikula vipande vinne vya madonge
vilivyotengezwa na maharagwe lakini
hakupendelea ladha yake'',alisema na
kuongezea kuwa ni Umar pekee aliyeendelea
kula.

Baadaye alisema kuwa alimuona bwana Sani
katika bustani ,akiwa mgonjwa na kumpeleka
nyumbani.
Lakini alipokuwa akijaribu kumuuguza bwana
sani ,aligundua kwamba watu wengine watatu
ambao walikuwa wamekula chakula hicho
wamefariki kwa ghafla.
Viongozi wa mashtaka walidai kwamba chakula
cha Tasiu kilichowekwa sumu kiliwaua watu
wanne na hivyobasi kuwajumuisha wanne hao
katika kesi moja ya mauaji.

Nigeria haijawahi kumyonga mtoto aliyefanya
uhalifu tangu mwaka 1997,ambapo taifa hilo
liliongozwa na dikteta Sani Abacha,kulingana
na shirika la kibinaadamu la Human Rights
Watch.

0 comments:

Post a Comment