Wazazi wengi Afrika wamekuwa hawajali
kuvitambua vipaji vya watoto wao kipindi wanapokua kwenye hatua ya utoto
na wanapoanza kukua, mfano mzuri ni kwamba ukiongea na watu ambao wana
vipaji na uwezo mkubwa kwenye mchezo kama mpira wa miguu, ama kuimba na
vinginevyo utagundua kwamba jitihada binafsi zimewaongoza kugundua
vipaji vyao na mchango wa wazazi ni mdogo ama usiwepo kabisa.
Hot news kutoka Coventry, Uingereza inamhusu Ayan Qureshi
ambaye ana umri wa miaka sita tu, na mwaka jana aliingia kwenye list ya
watoto waliofanya maajabu ambapo alifanya mtihani wa kampuni ya
Microsoft unaothibitisha wataalamu wa IT duniani na kufaulu, baba yake
ambaye ni mtaalamu wa IT anasema alimfundisha mtoto wake kuhusu masuala
ya Kompyuta tangu akiwa ana umri wa miaka mitatu.
Katika mahojiano na mtoto huyo amesema
mtihani ulikuwa mgumu lakini alienjoy kuufanya na alijiandaa kwa miezi
mingi kabla ya kuufanya, kutokana na kufaulu mtihani huo kwa sasa
anakuwa ni mtaalamu wa IT aliyethibitishwa na Microsoft ambaye ana umri
mdogo zaidi duniani.
0 comments:
Post a Comment