Mahakama Kuu imesimamisha mjadala wa
Ripoti ya Escrow kujadiliwa Bungeni
- Zitto asema taarifa ya PAC italetwa bungeni
hata zuio likiwekwa, awataka majaji wasome
Katiba na Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka
ya Bunge
BantuTz.con tumepata taarifa muda huu kutoka kwa mtu
aliyeko Mahakama Kuu kuwa kutokana na
taarifa iliyokuwa inaelezwa kuwa jopo la
majaji watatu wa Mahakama Kuu watasikiliza
kesi iliyofunguliwa na IPTL na PAP kuzuia
bunge kujadili suala la Escrow.
Imeamriwa na Mahakama Kuu chini ya jopo
la majaji watatu kuwa wamesimamisha
mjadala wa Ripoti ya Escrow hadi hoja za
msingi zitakapo fanyiwa kazi.
Mh. Zitto Kabwe ameandika yafuatayo katika akaunti yake ya Twitter na Facebook.
Zitto Kabwe-Facebook
"Bunge haliwezi kupewa zuio wakati mkutano
ukiendelea. Injunction itoke au isitoke Taarifa ya
PAC itaingia. Majaji wasome Katiba na Sheria ya
Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge"
"PAC inawahakikishia Watanzania kuweka ukweli
wote kuhusu uchunguzi wa akaunti ya
# TegetaEscrow . Tutawasilisha ripoti yetu
Bungeni kesho mara baada ya kipindi cha
maswali.
Narudia, tutatenda Haki. Aliyemo hatutamtoa na
asiyekuwemo hatutamwingiza. Mola atuongoze
katika kutenda Haki, kusema kweli na kweli tupu"
@Zittokabwe-TWITTER
"Parliamentary supremacy. With or
without court injunction Parliament will
debate #TegetaEscrow by PAC. No
constitutional crisis but a test"
Endelea kutembelea www.bantutz.com tutakuketea kila kitakachokuwa kinajiri.
"HAKI ITENDEKE,NA IONEKANA KUTENDEKA" LORD DENIN.
0 comments:
Post a Comment