Facebook

Wednesday, 26 November 2014

LIVE FROM DODOMA-SAKATA LA ESCROW

5:3O ASUBUHI
BUNGE LIMEHAIRISHWA MPAKA SAA 11:00 JIONI

Mh Kafulila kazungukwa na wabunge wengi sana nje wanampongeza kwa kuoa.


5:25 ASUBUHI

 MIONGOZO
(Nchambi):
Kuna taarifa mahakama imepinga kujadili Escrow (anazomewa sana na mwenyekiti anaomba order kwa tabu sana na anasema kila atakaeomba muongozo leo atapewa nafasi
na anatoa tishio la kusitisha bunge kama makelele yanaendelea) swala liloenda mahakani pia linamuhusisha pia mjumbe, kwa kua mjumbe huyu kamati kuu CHADEMA ameenda kuomba swala hili lisijadiliwe bungeni, CHADEMA wameonyesha wanapinga swala hili, tumjadilim pia na mjumbe.

Lissu: Huyu mtu ni mwanaCCM(Wakili wa PAN Afrika), mimi nimesoma nae na ndie alieua mke wake na kesi ikafutwafutwa na mimi nimesoma nae, ni kweli anafanya kazi na Mabere Marando lakini Marando hajausika. Hoja yangu mahakama kuu kutoa zuio bungeni tangia mahakama kuu ianzishwe mwaka 1922, ibara ya nne ya katiba kuhusu mgawanyo wa madaraka kwa mihimili imekiukwa(Makelele mengi na miongozo). Bunge lina uhuru wa majadiliano hivyo bunge liendelee na mjadala

Sendeka: Kutakua na uhuru wa mawazo kwenye bunge kwa mujibu wa katiba na hakutakua na chombo chochote kitachoweza kukabili likiwemo bunge. Nchi nzima inasubiri bunge kujadili ripoti bila ushabiki wa vyama vya siasa.

Khalifa: Tuna hofu ya nini, spika alichosema jana ilikua ruling ya bunge, tunachosubiri hapa ni ripoti tujadili

Deo: Spika alisema jana taarifa ya mahakama haipo, nadhani tuendelee kujadili bila kupoteza kwenye miongozo

Wabunge wanahitaji haki ya kujiandikisha kupiga kura

Bulaya: Niliwaambia mahakama zinatumika vibaya, waliofungua kesi ndio watuhumiwa. Mimi mbunge wa CCM siwezi kumlinda waziri, ilitwe ripoti ijadiliwe kila mtu abebe mzigo wake.

Msigwa: Tuliomba muongozo kuhusu briefing, ofisi ya spika inaendeshwa vipi

Nassari: Tunahitaji ripoti tuanze mjadala, na habari ya vyama vya siasa ikome

Lekule: Jana spika alitoa rulling bunge linaendelea, tunasubiri taarifa ya PAC wala mjadala huu haupiswi kuwepo, tufate order paper

Mwenyekiti: Kwenye order paper Escrow ipo, taarifa ya kiti bado bunge halijapokea barua yoyote kwa mjadala wa Escrow, nasitisha shughuli za bunge mpaka saa kumi na moja jioni
)

==========================================================================

5:06 ASUBUHI
Mzozo waanza bungeni,Muongozo ukiombwa

==========================================================================

5:05 ASUBUHI
BAADA YA MUDA WA RIPOTI KUSOMWA NA ZITTO KABWE KUSOGEZWA MBELE

HIVI SASA RATIBA INAYOENDELEA NI MUDA WA MASWALI NA MAJIBU

Swali: Lini mkandarasi ataanza kufanya survey
Jibu: Itategemea na upatikanaji wa pesa lakini tumeshawaagiza TANESCO wafanye survey

Swali: Unyapaa juu ya wagonjwa wa HIV, Kwanini kuwe na milango na madirisha ya dawa tofauti kwa wagonjwa wa ukimwi na wagonjwa tofauti, Je! sio unyanyapaa?
Jibu: Serikali kupitia wizara ya afya inatoa tiba bila malipo kwa hospitali zote nchini, Natoa wito kwa wanaoishi na VVU kujiandikisha ili kupata huduma. Milango ni tofauti ili kuimarisha huduma.

Swali: Vijana na vikundi vya uporaji, serikali inaelewa tatizo
Jibu: Serikali inajitahidi kudhibiti makundi yanayoibuka, nawaomba kuwashawishi wananchi kujiepusha na watu waovu na watoe taarifa polisi.

Swali: Jeshi la polisi halina vitendea kazi
Jibu: Ni kweli Polisi wanafanya kazi katika hali ngumu kutokana na ufinyu wa bajeti, tunaiomba serikali iongeze bajeti.

Swali: Ongezeko la ujambazi wa silaha Zanzibar baada ya kuondolewa hati ya kusafiria
Jibu: Kuondosha hati ya kusafiria Zanzibar kulifanywa kisheria, tafiti za karibuni matukio hayo yamepungua


==========================================================================


4:50 ASUBUHI
Dodoma hapatoshi zuio lakutokujadiliwa sakata la Escrow limeletwa na ndege asubuhi hii kutoka mahakamani na ndio maana kimeitishwa kikao cha dharura cha kamati ya uongozi akiwamo mh.Spika kwasababu hiyo inasemekana Mh Zitto asiwasilishe ripoti tena ....
TUVUTE SUBIRA...


==========================================================================


4:40 ASUBUHI
Mda huu sauti zaingiliana Bungeni mzungumzaji akiendelea kutoa maelezo ya majibu kwa wabunge ....huku sauti za wabunge wanawake ambao inaonekana hawajazima vinasa sauti vyao walikua wanapiga stories bila wao kujijua kama wanasikika wamesikika wakisema Mh. Kafulila yupo katika wakati mbaya kuliko kipindi chochote huku ndoa yake ikiwa ni changa na kuna uwezekano mkewe akamuacha Eda....sijaelewa maana ya Eda ni nini? Waliendelea kupiga stories bila kujua kama wanasikika kwenye mic Zao..... Mungu amlinde Kafulila



==========================================================================


4:25 ASUBUHI
*Yabainika: Serikali imesisitiza amri ya Mahakama itekelezwe ili #TegetaEscrow report isisomwe Bungeni *UPDATE: Serikali (Lukuvi na wenzie) wanadaiwa kutumia mabavu #TegetaEscrow Report isomwe tu bila kujadiliwa! *UPDATE: Watu wa PAP na hati yao ya mahakama wapo getini Bungeni wakitaka kutoa hati kwa BUNGE. BUNGE limegoma kupokea! #TegetaEscrow *UPDATE: Spika & Katibu wa Bunge wamejifungia ofisini kwa spika kujadili kabla ya Kamati ya Uongozi. Wenyeviti wengi hawajafika #TegetaEscrow *UPDATE: Wenyeviti Waliofika mpaka sasa ni Ngwilizi, Msola, Mbowe na Serukamba #TegetaEscrow

 
==========================================================================


3:25 ASUBUHI
Kamati ya Uongozi imekutana sasa hivi

Bunge limeanza na aliekalia kiti leo ni mwanyekiti wa bunge, mheshimiwa Zungu kuna maelezo juu ya malalamiko ya walimu, maelezo yanatolewa na upande wa serikali

Swali: Wapo watumishi kama wauguzi inadai zaidi ya milioni 100, japo kulikuwa na ahadi swala hili litashuhulikiwa, lakini hadi leo, nini kauli ya serikali?


Jibu: Hospitali ya tumbi ilipandishwa hadhi lakini bado haimudu. Mpaka sasa serikali imeshatoa bilioni tano kwa ajili ya jengo la upasuaji na baadhi ilinunua dawa. Serikali katita bajeti ya sasa imetenga pesa zaidi ili kufanikisha jengo la upasuaji

Swali(Zainabu): Ni lini serikali itatoa pesa ili hospitali ya Tumbi ikamilishe ujenzi? Lini hospitali za wilaya zitaweza kujitegemea kulingana na jiographia mkoa wa Pwani ngumu kwenda Tumbi

Jibu: Jambo linafatiliwa na namuhahakishia Mbunge tunafatilia fedha. Ni jambo la msingi tu tunazingatia kuzipa uwezo hospitali za wilaya

Swali (Mariam): Serikali ina mpango gani kuhahakisha Tumbi inapata madaktari bingwa kutukana na ajali
Jibu:Wizara ya afya ina mpango na madaktari washapatikana MOI na watasambazwa ikiwemo hospitali ya Tumbi



==========================================================================



Habari wWadau wa Bantu,
3:20 ASUBUHI
 Moja kwa moja kutoka bungeni Dodoma, leo tunaanza safari yetu yetu ya hitimisho kuhusu Escrow, japo kuna zuio la mahakama jana spika alisema bunge lina kinga na hakuna atakaezuia bunge lisijadili ripoti. Zitto pia amesema kamati ya PAC itawasilisha ripoti yake kama ratiba ilivyosema. Baada ya pilikapilika za usiku Dodoma tusubiri kitachojiri bungeni leo.

Hakikisha kifaa unachotumia kutembelea BantuTz.com kina chaji ya kutosha kutokana na hofu ya TANESCO pia kifurushi chako kiwe kinatosha kuperuzi hii kurasa mara nyingi iwezekanavyo.




8:56 USIKU
Hapo jana Ziito Kabwe na kamati yake walikesha wakilinda na kusubiri hadi asubuhi ya Leo waweze kuwasilisha ripoti yao kuhusiana na sakata la IPTL.






 

Tutakuletea moja kwa moja kila kitakachokiwa kinajiri kutoka bungeni mjini Dodoma katika kikao cha leo ambapo sakata la IPTL litakuwa linajadiliwa huku kamata ya PAC itakuwa ikiwasilisha ripoti yake.





0 comments:

Post a Comment