Mwanamke mmoja raia wa Uholanzi
amewasili nchini Uturuki baada ya safari
iliyojaa hatari nchini Syria kwa ajili ya
kumchukua binti yake aliyekua mjini
Raqqa, mji unaokaliwa na waasi wa Islamic
State.
Monique alikwenda Uturuki mara ya kwanza
baada ya binti yake aitwae Aicha kusafiri
kwenda Syria kuoana na mmoja wa
wanamgambo wa kundi hilo mwenye asili ya
Uholanzi na Uturuki.
Mamia ya Wanamgambo wenye asili ya Ulaya
wamekua wakienda Syria kupigana ndani ya
kundi la IS.
Aicha ,19 ni miongoni mwa Wasichana ambao
walisafiri kujiunga na IS.Raia wawili wa Austria
wenye umri wa miaka 15 na 17 walikwenda
Syria Mwezi Aprili na mmoja wao aliripotiwa
kuuawa.
Aicha aliondoka Uholanzi mwezi Februari,
akaolewa na Omar Yilmaz, mwanamgambo
mwenye asili ya Uturuki na Uholanzi ambaye
alishawahi kuwa mwanajeshi nchini
Uholanzi,alitumia mbinu alizopatiwa akiwa
mwanajeshi na kuwafunza wapiganaji wenzake.
Monique amesema mwanae alibadilika ghafla
kutoka binti aliyefahamika vyema na kuwa
Msichana mwenye msimamo mkali.
0 comments:
Post a Comment