Zitto alikuwa kamchapa Spika Kiufundi

Ilikuwa hivi;Bunge lilifikia ukomo wa mjadala na kutakiwa kufanya maamuzi.

Wakawa wanatafuta lugha gani ikitumika haitaonyesha Bunge kuingilia Mihimili mingine kama Serikali na Mahakama.

Walipofika kumuwajibisha Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini mvutano ukawa mkali.

Ndipo Spika akamteua Chenge atoe mchango wake.

Chenge akasema.

"Bunge linapendekeza Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Kichukuliwa hatua na Mamlaka za uteuzi"

Wabunge wengi hasa wa upinzani hawakuridhishwa si tu na maelezo hayo bali hawakuwa na imani hata na alie kuwa anayatoa maana yeye ndio KUBWA LA MAADUI,ndipo Spika alipo Mtaja Mh Zitto ambae kwa karibu sana alikuwa akishauriana na Halima Mdee.

Ndipo Zitto akasema

"Nashauri tuikubali sentensi(maelezo)iliyosema na Mh chenge itumike kwa mapendekezo ya kamati yaliyobaki.

Kimbuka pendekezo hilo lilikuwa pendekezo nambari saba.

Pendekezo namba 8,9...yalihusu kuwajibishwa Masele,Muhongo,na Pinda.

Spika kwa kutokukua mtego wa Zitto uliolenga Mamlaka ya uteuzi imuwajibishe mpaka waziri mkuu ambae Spika amejipanga kumlinda kwa nguvu zote,

Spika akaona apige kura haraka haraka,kama kawaida ccm wakasema Ndiyoooo......


Punde tu Ole Sendeka ambae nae anataka wote wawajibike isipokuwa Pinda na Masele akashtuka na kumjulisha Spika haraka,wakati huo wapinzani karibu wote walikuwa wakilalamika kwa Spika kupigisha kura haraka haraka isipokuwa WENJE.

Ndipo Spika akagutuka na kurudi kwenye utaratibu wa mwanzo wa kipendekeza kwa kila mmoja

Wenje akaanza kumzonga Spika kuwa tumeshafanya maamuzi,na Maamuzi yalikuwa ni Ndiyo hivyo Spika asimamie maamuzi ya wabunge.

Hivi ndivyo Zitto alivyokuwa kamaliza Mchezo kirahisi kwa wale waliomuelewa,lkn wengi hawakumwelewa alichokimanisha.

Pamoja na hayo bado wote kwa umoja wetu hatupaswi kuondoka kwenye hoja ya msingi ambayo nikuona wezi wanawajibika.

Kesho Bunge litaendelea saa tatu asubuhi.