Facebook

Sunday, 23 November 2014

Mama Anne Kilango Malecela azushiwa ugonjwa wakati ni Ni Mzima Wa Afya

Kumekuwa na uvumi unaosambazwa na genge la wahuni katika siasa kwamba mbunge wa jimbo la Same Mashariki ndugu Anne Kilango Malecela kuwa anaumwa sana.Wanaozusha maneno haya wanaenda mbali zaidi na kusema afya yake imedorora sana.

Ukweli wa mambo uliopo ni kwamba Mama Kilango ni mzima wa afya.Haumwi ugonjwa wa aina yoyote ule.Mama Kilango anaendelea na majukumu yake kama kawaida.Anahudumia wananchi waliomchagua kama ilivyo kawaida yake.Kwahiyo uzushi huu tuukatae kabisa.

Pia inavumishwa kwamba Mama Kilango amekuwa kimya sana kuongelea suala la Escrow wakati ni kawaida yake kukemea uozo serikalini.Katika hili jamii inapaswa kujua kwamba Mama Kilango hayupo kimya katika kukemea ufisadi wa Escrow.Anachosubiri ni taarifa ya vyombo husika juu ya sakata hili.Pindi akipokea ripoti atakuwa katika nafasi nzuri ya kupaza sauti yake kwasababu haamini katika kuropoka bila ushahidi.

Mama Kilango ni msomi wa shahada ya uzamili ambapo kikawaida itakuwa ni ajabu kwa msomi wa aina yake kuzungumzia jambo lolote lile bila kuwa na ushahidi usio na mashaka.Kwahiyo ukimya wake katika sakata la Escrow ni kwasababu anasubiri aipokee ripoti.

Wananchi wa Same Mashariki na Tanzania kwa ujumla mnapaswa kuwa na imani na Mama Kilango.Kataeni ujinga unaoenezwa juu yake.Ni mzima wa afya na pia katu hawezi kukalia kimya ufisadi wa aina yoyote ile.Mama Kilango anaipenda nchi yake na kukipenda chama chake.Anaiheshimu serikali yake pia.Hawezi kuwa sehemu ya waliochangia kuanguka kwa serikali kwa skendo za kuzusha.Anamheshimu waziri mkuu na rais pia mawaziri na manaibu waziri wote Tanzania.

Kwa kuhitimisha,niwaombe radhi wananchi wa Same Mashariki na Tanzania kwa ujumla kwa usumbufu uliojitokeza.Mama Kilango atazungumza muda ukifika.Aliikataa Richmond hivyobasi ataukataa ufisadi wowote akipata ushahidi.Mafisadi kwake ni adui namba moja.Anawaasa muikatae rushwa na muwakatae mafisadi katika jamii.

Mbarikiwe sana.

0 comments:

Post a Comment