Jana tulikuwa tunamalizia ngwe yetu ya mwisho bungeni, baada ya wasilisho la ripoti
ya PAC, majibu ya serikali na mjadala wa wabunge wa jana, moja kwa moja
kutoka Dodoma tuwe pamoja kuimaliza ngwe yetu. TANESCO wameshatoa
tangazo rasmi la matatizo ya umeme hivyo chaji zetu ziwe vizuri nafasi
ya kupata umeme inapopatikana.
=============
Spika ana Makinda ndiye aaliekalia kiti leo na Mwanri anajibu maswali yanayohusu wizara ya afya.
Mangungo(Nyongeza): Eneo la Mlandizi ni eneo la barabara kuu,
nini ahadi serikali kuharakisha upatikanaji wa kituo ili kuwapelekea
wananchi huduma karibu? Lipo tatizo la wahudumu wa afya na madaktari
japo majengo yapo, nini jitihada ya serikali?
Mwanri: Nakubaliana eneo la barabarani ajali nyingi, tutajitahidi
kukamilisha haraka na kuona inafanyiwa kazi. Kuna vibali vimetoka kwa
wahudumu wa afya pia wizara pia inapeleka watumishi moja kwa moja.
Tuliwapa nafasi cha watumishi 8,000 wizara ya afya pia tumewapa kibali cha watumishi 1,000 na bado hakijamaliza.
Suzan Lymo: Maslahi ya walimu lazima yaboreshe, serikali inafahamu tatizo
Mwanri: Nakubaliana lazima kuboresha maslahi ya walimu, tuna
upungufu wa walimu na nyumba za walimu. Mkakati wa serikali na pamoja na
kudahili walimu na maabara, nyumba za walimu na kuimarisha mfumo wa
kuwahudumia walimu.
Suzan Lymo: Kuna tatizo la upangaji walimu kwa shule za
pembezoni, pia watendaji wanakaimisha walimu majukumu badala ya kukaa
kwenye vituo vyao vya shule
Mwanri: Kwanza kweli kuna tatizo, lakini tatizo kwa walimu wa
sanaa limpembukua sana, tutafanya upangaji(re-allocation). Mwalimu kazi
yake ni kufundisha hivyo kuwapa kazi za watendaji haikubaliki.
Leizer: Ni lini serikali itachukua mkakati kwa nyumba za walimu kama walivyofanya maabara!
Mwanri: Jitihada za maabara tunazipongeza halmashauri, kuna
halmashauri tumewapelekea milioni 500 kila moja ambazo zipo katika
mazingira magumu.
===============
Maswali sasa ni kwa Wizara ya Nishati na Madini, ambapo
maswali yanajibiwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Stephen
Masele.;
Mhe. Mbilinyi: Tunazungumzia sana mafanikio ya kusambaza umeme,
kuna umuhimu gani wa kuendelea kusambaza umeme wakati huwa unakatwa
kwenye nyakati maalum. Mfano; Jana kwenye mjadala wa Escrow?
Jibu: Tutofautishe kati ya kuwapatia umeme wananchi na kupatikana
umeme wakati wote. Jana kulikuwa na hitilafu ndogo tu, ila Leo mbona
umeme upo.
Mhe. John Komba (nyongeza) : Katika Maeneo ya Mbamba bay, kwanini umeme mpaka sasa haujafika kama ilivyoahidiwa?
Jibu: Kuna Matatizo ya nguzo, kutokana na demand kuwa kubwa sana
wakandarasi wameagiza nguzo za kutosha ili kuhakikisha miradi yote
inakamilika.
Maswali kwa wizara hii bado yanaendelea....
============================== =========
Sasa ni zamu ya maswali kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi;
Swali: Ni lini serikali itaboresha magereza kwa kuwa yapo kwenye hali mbaya kwa uchakavu, pamoja na miundombinu yake mibovu?
Jibu (Naibu waziri) : Serikali kupitia wizara yangu, ipo kwenye mikakati ya kutatua changamoto hiyo.
Swali: Hivi karibuni, nchi jirani ya Kenya tukio la westgate
lilitishia usalama wa nchi na raia wake, Je serikali imejipanga vipi
kuzuia tukio kama lile lisiikumbe Tanzania?
Jibu: Tukio la Westgate la Kenya, lilikuwa ni tukio la kupangwa
likihusisha masuala ya ugaidi. Serikali ya Tanzania kupitia jeshi la
polisi, linajitahidi kwa makusudi kukusanya taarifa za kiintelijensia na
kuimarisha ulinzi.
==================
Maswali kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia;
Swali: Ni kiasi gani makampuni ya simu za mikononi zimelipa Kodi kwa Mwaka uliopita?
Jibu: Makampuni ya simu hulipa kodi kwa utaratibu uliowekwa. Aina za kodi ni pamoja na VAT, Service, Corporate TAX na nyinginezo.
Swali Nyongeza: Hivi karibuni serikali imeweka mtambo wa kudhibiti simu zinazoingia na kutoka nchini. Je, imeongeza vipi kodi (pato)?
Jibu: Ni kweli serikali imeweka mtambo wa mawasiliano pale TCRA,
Mtambo huo una kazi zake mbali mbali. Lakini kwa sasa serikali
imefikiria namna ya kupata solution ya kuangalia namna gani itakagua
mobile money transfer ili kuweza kutoza kodi.
Swali nyongeza (Zungu): Mheshimiwa waziri hujatoa majibu ya
kitaalamu, kwani mtambo huo bado kabisa haujaanza kufanya kazi kama
inavyotakiwa kufanya. Sasa nauliza, ni lini software hii ya kutoza
wafanya biashara hasa wa mitandao ya simu italetwa na kuanza kufanya
kazi ili mwananchi ajue kodi yake inaenda serikalini moja kwa moja?
Jibu: Kwa sasa mtambo unafanya kazi ya kukagua simu zinazoingia
na kutoka, za kihalifu pamoja na kukagua mawasiliano kwa ujumla. ILa
Tunaamini mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu kazi hiyo itakuwa
imekamilika.
===================
Maswali na Majibu kwa Wizara ya Fedha;
Swali (Prof Makyusa): Tangu kuanzishwa kwa VICOBA wananchi wamenufaika sana, Je Serikali inaitambua VICOBA kama ni mkombozi kwa wananchi vijijini?
Jibu (Mwigulu): VICOBA ni miongoni mwa taasisi ndogondogo za
fedha zinazoanzishwa ili kutatua changamoto za kifedha kwa wananchi
hususan wa vijijini. Taasisi hizi husimamiwa na wananchi wenyewe. VICOBA
si taasisi ya Serikali, bali ni ya mtu binafsi. Kwahiyo wizara haina
bajeti kwa taasisi ya VICOBA.
Swali la Nyongeza: Kwa kuwa VICOBA si taasisi ya serikali na
serikali haina bajeti kwa ajili ya taasisi hizi ndogo ndogo, Kwanini
sasa isifikirie namna ya kuboresha na kuziwezesha hizi taasisi za
microfinance kwa kuwa ni jambo jema?
Jibu: Serikali itajitahidi kupitia miradi ya maendeleo, kufikiria
namna ya kuweza kuwezesha VICOBA, pamoja na kutoa mafunzo kwa wananchi
wanaoishiriki kwenye VICOBA, Serikali pia inafikiria kuifanya VICOBA
hatimaye kuwa rasmi kama hatua kubwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi
kujitegemea.
=========================
Ni zamu ya Maswali kwa Wizara ya Kilimo na Chakula;
Maswali yanaulizwa kuhusu kukosekana kwa pembejeo katika
baadhi ya vijiji na wilaya, Na Wizara inajibu kuwa zoezi la kutoa
pembejeo limeanza, labda Mawakala wanafanya zinachelewa kuwafikia
wananchi, Hata hivyo wizara inadai itafuatilia.
============================== ====
Maswali kwa Wizara ya Maji;
Swali (Mhe. Mbilinyi): Tatizo la kukatika kwa maji na kukosekana katika maeneo mengi ya mbeya, linasabishwa na nini?
Jibu: Kukatika maji kunasababishwa na kukatika kwa umeme mara kwa mara. Hivyo ni changamoto ambayo inafanyiwa kazi.
Swali la nyongeza: Kuna tatizo la bili pia. Wananchi wanalalamika bili ya maji huja kwa bei ya juu tofauti na malipo ambayo hufanywa mara zote.
Jibu: Swala la bili huwa inatokea. Tutaliangalia hilo kwa umakini mkubwa.
============================== =
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi;
Swali (Nyangwine): Lugha ni nyenzo muhimu katika
kujifunza, kwanini lugha ya kiswahili isitumike kama nyenzo rasmi ya
kujifunzia?
Jibu: Lugha ya Kiswahili na kiingereza zinatumika kwenye kujifunza, hata
hivyo suala hilo litapewa kipaumbele kwa kuwa Kiswahili ni lugha ya
kipekee.
Maswali machache yanafuatia. Majibu yanatolewa.
================
Mwisho ni Maswali kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi;
Maswali yanaulizwa kuhusu sheria ya ardhi inayozungumzia ulipwaji
wa fidia kwa wakazi wanaoathiriwa na uchimbaji au matumizi makubwa ya
ardhi kwa maeneo husika. Ikiwemo kuwapa makazi mapya pamoja na fidia
kulingana na thamani ya bei husika.
Wizara inajibu kuwa ni kweli, na sheria iko wazi. Isipokuwa kipengele
cha ujenzi wa makazi mapya hakikuandikwa kwenye sheria lakini ni jambo
la kufanyiwa marekebisho tu.
============================== ==============
UTAMBULISHO WA WAGENI NA MATANGAZO YA KAZI
============================== ==============
Mkono ameomba kuwa kwenye sehemu ya wachangiaji baada ya Muhongo kumuhusisha jana.
MJADALA
Nchambi: Anailaumu serikali kwa kuchelewesha kuleta jambo husika
bungeni, watanzania wana hamu ya kujua fedha ni nani? Wakili wa
TANESCO(Mkono) alishauri kufunguliwa akaunti(ananukuu maandiko ya biblia
kuhusu kuheshimu mamlaka), anasema kila mtu atawajibika kwa namna yake.
Hasara nyingine tuliyoipta ni gharama za mawakili(bilioni 62) ambayo
watuwengi hawaigusii, kesi imeenda miaka kumi hivyo haki kupatika
ilionekana ni ngumi na bado tunadaiwa. Baada ya malipo tutakuwa
tumepoteza bilioni 90 kwenye kesi.
Lazima tuangalie pande zote mbili, sehemu serikali inapotakiwa
kuwajibika pia watu binafsi watatakiwa kuwajibika, fedha baada ya kutoka
escrow na maamuzi(ruling) kutoka. Ilionekana bado TANESCO bado
ingedaiwa lakini lazima serikali ituletee majibu dhidi ya mgogoro wa
capacity charges.
Wizara ya nishati na madini ilikuwa na matatizo mengi kabla ya Prof
Muhongo, tunapojadili hoja tujadili yenye mashiko. Tanzania ina kata
3804, Muhongo ameingia katika bajeti moja na kusambaza umeme vijiji
vingi (ananukuu Quraan kuhusu kusema kweli).
Ananukuu Biblia watu wasiwe wakorofi(kumuingilia wakati anaongea), fedha
za Escrow sio ugomvi ya ubadhilifu wa fedha pekee. Bei ya umeme
tunaouziwa imeshika baada ya Muhongo, anasema kunaweza kuwa na chuki ya
kibiashara hivyo tutumike kwa masilahi ya nchi na sio wafanyabiashara.
Kuwatisha wawekezaji sio jambo jema na tutapoteza imani na wawekezaji,
waliotajwa kuhusika na fedha hizo serikali iwachunguze. Wapo watu
wameingiziwa fedha kwenye akauti zao. Ananukuu Quraan kuhusu haki na
batili, anapata mashaka mbunge kwenda kukagua wakati yeye pia anatiliwa
mashaka. Kuna list ya watu itakuja hapa bungeni, kuna watu wa kambi ya
pili wametetea hili jambo kwa upole na unyonge. Wabunge tusimamie haki
na tuseme ya kweli, tulianza na Mungu na tuendelee na Mungu. Anamsifu
Muhongo kwa kazi anayoifanya wizarani. Waziri mkuu ametajwa, ametajwa
kwa namna tofauti na kuna watu ni majeruhi. Ananukuu Quraan kuhusu
wajuzi, niwatie moyo mjadala uende vizuri.
Mwigulu Nchemba: Ukububwa wa jambo tunaongelea maadili na maslahi
ya watanzania, nitajikita eneo linalogusa wizara ya fedha. Nazipongeza
taasisi zote zilizoshiriki kwenye ripoti hii(anazitaja). Tangu utaratibu
huu uanze, chimbuko la ripoti hii ni serikali yenyewe.
Kodi, imegawanyika maeneo matatu, VAT haikukatwa na kukatokea
mkanganyiko, TRA inashughulikia na ni ilikua ni bilioni 26.97 lakini
baada ya kugundua kuna kodi ya wananchi haijakusanywa ndipo wakakusanya
bilioni 4.1 na ukaguzwa ni wa kwenye Escrow na sio IPT. Niwahakikishie
watanzania kuwa kodi hii italipwa, hatuwezi kuacha kodi kwa tajiri
halafu tukimbizane na mama mjane anaeuza mchicha barabarani.
Kodi ya pili ni iliyotokana na kukosewa kwa mahesabu na ni lazima
ilipwe, TRA imeshaandika barua ya Novemba 2014 ya kufuta
cheti(certificate). Brela wameshapewa notice ya kufuta capital gain
certificate iliyotolewa kipindi kilichopita. Hatua imechukuliwa na
serikali na tuko makini. Kuna watu wasio waaminifu, kuna mtu badala ya
kuandika $ milioni 6 akaandika Tshs milioni 6 na badala ya kuandika
$milioni 20 ameandika Tshs 20. Naagiza mamlaka ya TRA ifanye
uwajibishaji wa ndani na akafanye kazi nyingi na hakuna uchunguzi juu ya
uchunguzi. Mtu aliyeiba ukimfukuza kazi ni kumpa likizo akatumie fedha
alizoiba hivyo mamlaka husika wachukue hatua. Tumeambiwa kuhusu pesa
zilizogawiwa, na wenyewe walipie kodi kabla ya tarehe 31/12/2014. Baada
ya tarehe hio TRA wafatilieni mmoja mmoja. Kuna taarifa pesa zilitoka
kwenye mafurushi na magunia, nimefatilia na wamefata sheria. Anatoa
agizo kwa Stanbic na Mkombozi watoe matamko, wateja wao wana haki ya
kujua reputation ya benki yao. Niwaombe wabunge, kuna kuongea na
kuchukua hatua na watanzania wanasubiri kuchukua hatua. Tumekua
tunawachukulia hatua wanasiasa lakini wataalamu waliosomeshwa kwa kodi
hawajibiki popote.(Muda umeisha)
Kafulila: Benki ya stanbic wamemfukuza kazi aliefungua akauti ya PAP
amefukuzwa kazi asharudi kwao Uganda hivyo hizi ni dalili kuwa kuna
makosa yalifanyika ndo maana hatua zimechukuliwa.
Mnyaa: Nampongeza Nchemba kwa kusimama katika ukweli, economic
hitman ni kama Mafia, na washawahi kuziangusha nchi(anazitaji) na miradi
mikubwa wanayohusika nayo ni kama ya umeme, tujiulize kama hawajaingia
Tanzania. Nyaraka nyingi zilizothibitishwa akatoa mbunge kuzikanusha ni
kosa, Muhongo anasema ana nyaraka muhimu kwannini hakuzipeleka kwa CAG,
maadili ya viongozi ambayo katika maazimio ya Richmond yaliazimiwa.
Mwanasheria wa RITA leo yupo katika IPTL na mgao. CAG anapinga wabunge
kuwa wajumbe wa bodi, leo hii sio conflict of interest? Wahusika ni IPTL
na TANESCO na BoT NI MSIMAMIZI.
Imekuwaje BOT kutuma pesa PAP badala ya IPTL, kwa nini imekiuka akouti ya Escrow.
Mchangiaji: Ni dhambi kudhania PAC ni chombo cha wapinzani, kama
kuna mapungufu ni bora tuyarekebishe, wanaofanya haya wanakula na
viongozi wetu wa juu. Katika hili wananchi wameathirika sana kutokana na
balaa hili la overcharge. Haiwezekana watu kuchukua pesa za dhulma na
sisi wanyonge kuzilipa. Hakuna yoyote aliye alie juu ya sheria,
uwajibikaji ni la lazima. Mbona alijiuzulu kwa mzigo wa watu wengine
kwakuwa walikuwa chini yake.
Ashumta Mshana: Kuna taarifa tatu, ya serikali, PAC na CAG ila
ukisoma zote zimetofautiana hivyo kutufanya tusielewe vizuri, taarifa ya
PAC ina mapungufu mengi. Mbowe ametajwa kupokea pesa lakini haijataja.
Taarifa: PAC inafanyia kazi taarifa ya CAG, hayo majina unayoyasema hayakuwepo.
Ashumta: Kwani mapendekezo ya PAC yapo kwenye taarifa ya CAG
Mwenyekiti: Si vizuri kutaja majina ambayo hayapo kwenye ripoti.
Ashumta: Benki ya Mkombozi pekee majina yake ndio yameletwa,
tunataka na majina ya Stanbic. Waziri mkuu hawezi kuondoka, tunao
uhakika mbele yetu. Ripoti ya CAG hakukuwepo kuwa Muhongo amehusika moja
kwa moja.
Waziri wa nchi: Kwa mujibu wa kanuni, nasogeza muda wa bunge mpaka saa nane mchana.
Nkumba: Serikali lazima ichukue hatua, haiwezakini ukapewa
bilioni na Lugemalila lazima aseme alitoa hizo fedha kwa ajili ya nini.
Nimshukuru Lugemarira ametusaidia sana kumaliza hili jambo hili. Hata
kama ni chama cha mapinduzi tuwashughulikie.
Sendeka: Hapa hamna uwajibikaji wa pamoja bali mtaje wahalifu,
wahalifu lazima wabebe, hakuna majina ya watu kwenye mauzo, huhitaji
akili kubwa kujua kuwa hapa kuna uhalifu, watu wamekwepa kodi bilioni
8.7 kwa watu kughushi, haihitaji upoteze muda, utajua hapa kuna utapeli
tangu mwanzo, kusimama na kusema ofisi ya CAG ni uongo mtaiambia nini
dunia kwamba vyombo vyetu vyetu tulivyoviweka ni uongo. Hii ni dhambi,
watu wanaopata fadhila za wizara wanakaa kwenye kamati. Muhongo kafanya
kazi ya udalali, watanzania ni vyema wakapata majibu kama ni kweli ama
la, kwenye mkataba unamtaja mheshimiwa Muhongo(anaunukuu)
Muhongo anaomba taarifa kuwa anachosema Sendeka ni uongo na
kilichoandikwa si lazima awe sahihi, niwahakikishie watanzania hakuna
mwekezaji yeyote nchi hii ambae hajaja kuonana na mimi.
Zitto: Nyaraka za CAG zimekua verified lakini za Muhongo alizozitoa uongo, mkataba unasema walikutanishwa na Sendeka.
Sendeka: Nimesoma kwenye mkataba ambao pia uko ofisini kwako na
wewe umeshiriki, profesa aliita nyaraka nilizozileta ni za kufungia
maandazi, hakuna shaka kuwa Muhonga alikua dalali katika dili hili, nina
uhakika miongoni walionufaika ni waliowezesha dili hili. Ingekuwa
haunizidi umri ningesema ulichofanya ni ukuwadi. Kodi la ungezeko la
mtaji kila mmoja anajua tulivyoibiwa, ushauri wa nwanasheria mkuu
umekwepesha kodi nchi hii, tunamlinda kwa sababu gani, Muhongo na Maswi
pia bodi ya TANESCO inabaki kwa sababu gani! Tulimwajibisha, waziri leo
anapewa masaa mawili kuitetea serikali ambayo si ya serikali bali wake
mwenyewe. Mlienda Kunduchi kugawana fedha kwa njaa. Isaidieni nchi hii,
hamuwezi kukwepa kodi alafu mkaja kutetea. Mwisho tupige kura juu ya
mambo haya. Hatujakokotoa na bado tukampa Lugemalira lakini alilipa
mabilioni ya kodi wakatiSeth mmemuacha. Mkono mlimpa dili wenyewe na
mwanasheria wa TANESCO mkamfukuza bila haya, mi naomba waziri mkuu
arudishwe. Huitaji kuwa msomi kujua. (Muda umeisha)
Lekule: Mhe M/Kiti, Hili suala tusiliwekee utani. Tusilizungumze wala
kulijadili kwa mzaha. Ni jambo zito tusilete siasa. Sio suala la CCM
kuiba fedha za UKAWA wala kinyume chake bali ni suala la wizi wa fedha
za Umma.
Kiwango cha fedha kilichoibiwa, ni kiasi kikubwa. Hatuwezi kusema hizi
pesa sio za umma, maana kuna fedha za kodi, hata kama pesa ni za
mashirika, lakini zina kodi ndani yake. Kwahiyo ni fedha za Umma kwa na
namna moja ama nyingine.
Akaunti ya escrow imeingiliwa na wezi wa aina mbalimbali. Leo tutafute sumu ya kuwapa hawa wezi wa hizi fedha.
Mhe. M/kiti, haya mabilioni yaliyogawanywa utashangaa, hivi huyu tajiri
aliyegawa hizi fedha,anataka nini kwa hawa watu wote hawa? Hata duniani
kote haijawahi kutokea tajiri akagawa pesa kwa namna hii.
Hizi fedha ni za jasho lake kweli? Maana haitegemewi fedha za jasho lake
kugawiwa kwa namna hii, Matarajio yake ni nini kutoka kwa hawa watu?
Mhe. M/kiti, TANESCO ni shirika la umma, kwahiyo kama kuna fedha za
TANESCO humo ndani tuna haki ya kudai. Kama ikishindikana
kutowawajibisha hawa waliohusika na wizi huu, basi ni bora waliotangulia
kama wakina lowassa, ngeleja na wengineo waje tuwaombe radhi, Kwa
sababu sioni tofauti ya hawa viongozi.
Kwa sababu sitegemi nipewe 1.6 bilioni bila kujiuliza, hizi fedha ni za nini?
Kwahiyo naomba uchunguzi ufanyike zaid. Mimi nawapongeza kamati ya PAC,
wamefanya kazi nzurri na bunge tuige kamati hiyo. Naomba na kamati
nyingine zitakazochaguliwa kufanya kazi kama hii waige mfano huu.
<<<<<<<TAARIFA>>>>
Lekule: Mhe M/kiti bado nasema, hii kazi tunayofanya tufanye kwa umoja
bila kumuonea mtu na tusilindane tufanye kama inavyotakiwa..(Makofi)
Asante sana.
====================
Mwenyekiti wa bunge, Mussa A. Zungu anaahirisha kikao cha bunge hadi saa
10 badala ya saa kumi na moja jioni, ili wachangiaji wawe wengi na
kupata muda wa kutosha.
Wachangiaji watakaoanza jioni ni;
- John Mnyika
- Halima Mdee
- Esther Bulaya.............na wengineo.
Asanteni.
==============
DONDOO MUHIMU KIKAO CHA JIONI
Kigwangalla: Sijawahi kuona Profesa muongo kama Muhongo
Kigwangalla: Toka lini pesa za watu binafsi zikawekwa Benki Kuu?
Mpina: Ni bahati mbaya tuna Profesa muongo kama Muhongo ambaye ni
Waziri wa Nishati na Madini. Pesa zilizotolewa hazijalipwa kwa mmiliki
halali wa IPTL, PAP sio wamiliki halali!. Mwanasheria Mkuu wa Serikali
aliingilia majukumu ya TRA ktk kukusanya kodi
Zitto: Nimekuwa na mgogoro na chama changu lkn kwenye hili wameniunga mkono, kwa mara ya kwanza nimehudhuria kikao cha UKAWA
Kuna baadhi ya wajumbe wanadai tumetumwa na Uingereza. Hakuna kinachonituma kufanya haya, ni uzalendo kwa nchi yangu
Mahakama ilikiri kuwa kweli tulikuwa overcharged; ikaamriwa yafanywe mahesabu upya!
Prof. Muhongo alisema anaheshimu mahakama za ndani. Jaji utamwa hakuwa anaamua kesi ya Escrow wala Capacity Charges
Jaji hakusema kokote kuwa toeni hela mkawape IPTL. Hakuna sehemu alikotaja kitu kama hicho
Kama TANESCO ina madeni makubwa na haina hela; Tanzania ina deni kiasi gani la Taifa? Basi tumeshauzwa!
Muhongo alikuta TANESCO ikiwa na hasara ya Bil 43. Sasa TANESCO ina deni la zaidi mara 4!
TRA wamegundua fraud kwamba nyaraka za PAP zilikuwa forged! Nchemba ameonesha ukomavu ktk hili
Hivi watanzania tumefikia hatua ya kuukata utanzania kabisakabisa?
Prof. Muhongo anadai yeye hahusiki na mambo ya makampuni. Sheria iliyotungwa mwaka 2012 haisemi hivyo!
Umeme umekatika Bungeni, wabunge wanashangilia!
Zitto: Kijana aliyesema Singh ni tapeli ametengenezewa kesi ya mauaji. Alifukuzwa kazi! Naomba apatiwe ulinzi
Zitto: Prof. Tibaijuka aliniandikia mchango wake wa maandishi kuelezea alivyopata fedha; tunawaachua Kamati ya Maadili
Zitto: System ili-collapse wakati wa mchakato wa uhamishaji wa mabilioni haya
Zitto: Tuhuma zikiachwa bila kufanyiwa uchunguzi watu huziamini. Naomba tuhuma za Lusinde kwangu zifanyiwe uchunguzi
Zitto: Naomba wanaonishughulikia wanishughulikie mimi; mwacheni mamangu apumzike (anatokwa machozi)
Kafulila: Tusiache kujadili kifo cha Waziri Mgimwa kisa mwanae hataki; kuna siku Rais atakufa na mwanae atataka tusichunguze
Chenge: Naomba neno KUFA listumike bali litumike neno KUFARIKI linakuwa na staha kidogo
Pendekezo la Serikali kumkamata Harbinder Singh Sethi kwa money laundering limekataliwa na Serikali hadi kesi iliyopo iishe
Lissu: Sethi akamatwe. Shauri lililopo mahakamani ni shauri la baadae! Akamatwe kwa sababu jinai kubwa imefanyika
Lissu: Pendekezo hili la serikali naomba wabunge wasilikubali; mtu huyu ahukumiwe kwa jinai
Simbachawene anapendekeza Sethi asikamatwe kama ilivyopendelezwa na Serikali; wabunge wanazomea
Mdee: Si ajabu kwa mtu mmoja kuwa na kesi ya jinai na kesi ya madai. Huyu Sethi afunguliwe kesi ya jinai
Halima Mdee: Kilicholetwa na Serikali ni ovyo, kinalinda wezi (kutaka Sethi asikamatwe mara moja)
Pindi Chana: Wa kukamatwa si Sethi peke yake; vyombo vya dola vifanye uchunguzi kwanza kubaini jinai iliyofanywa
Zitto: PCCB na TRA wameshafanya uchunguzi; mnataka vyombo gani vingine vifanye uchunguzi?
Werema: Eneo hili ndo litaleta mgongano mkubwa kati ya Bunge na Mahakama. Kwa sasa ni vigumu kusema "mkamate"
Makinda: Mnaposema akamatwe mnakosea, sisi siyo mahakama, tutafute njia nyingine na tuweke lugha ya kwetu siyo ya mahakama
==================
MAAZIMIO
Pendekezo la kwanza la kumkamata na kumfilisi bwana Seth lina marekebisho ya serikali, naibu waziri wa Sheria anasema haiwezekani
Pendekezo la pili kuhusu Rugemalira, serikali imeweka marekebisho kuhusu uhalali wa pesa za Rugemalira alizogawa
Azimio la TATU limerekebishwa kuwa waliopokea pesa wachunguzwe na kuchukuliwa hatua mahususi kwa mujibu wa sheria
Pendekezo la NNE. Kamati inazitaka mamlaka kuzitangaza benki za Mkombozi na Stanbic kama asasi za utakatishaji fedha
Azimio la 4 limepita kwamba Kamati inazitaka mamlaka husika ikiwemo benki kuu kuchukua hatua dhidi ya benki zote zilizohusika
Azimio la TANO: Serikali ipitie upya mikataba yote ya umeme na kutoa taarifa kabla ya kumalizika kwa Bunge la bajeti lijalo
Azimio la SITA: kuhusu Bodi ya TANESCO kuvunjwa kwa kusababisha pesa kuchotwa na hasara, serikali imekataa, mjadala unaendelea
Kingwangala: Kanuni zetu zinataka mtu yoyote anayetaka mabadiliko ya maazimio lazima awe amekawasilisha kabla
Kafulila: Kwa mujibu wa mkataba wa IPTL, maamuzi ya mwisho
yanafanywa na mahakama ya London, bodi walikuwa na maamuzi hayo na
haikuwajibika na maamuzi ya mahakama za ndani ya nchi
Majibu: ISCD ilisharidhia injuction ya mahakama ya Tanzania na
ikaijulisha standard charted hivyo si sahihi kusema ISCD ina mamlaka ya
mwisho, IPTL pia ilipata injuction kwenye mahakama za Tanzania
IPTL sio kampuni ya kimataifa tena bali kampuni ya ndani
Mdee: Bodi ya TANESCO, napendekeza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi vitendo vya jinai na kuchukua hatua kwa bodi ya TANESCO
Mbowe: Kazi yote hii pengine tusingefika hapa kama bodi ingekua
makini, bodi ya TANESCO haiwezi kukwepa lawama hii. Bodi ya TANESCO
iwajibishwe
Lissu: Maneno ya Mdee yanahusu jinai, ishu ni bodi ya TANESCO,
(Anapendekeza bunge livunje bodi ya TANESCO ivunjwe na iundwe upya
kuongeze ufanisi.
Shekifu: Tusifike mahala bunge likatoa amri lakini kutekeleza
shughuli pia tuna mihimili mitatu, bunge linaishauri tu serikali na
bunge haliwezi kuivunja bodi ya TANESCO
Azimio hili ni la bunge hivyo tuepuke kuvunja katiba
Zitto: Bunge linaelekeza kwamba bodi ya TENESCO liundwe upya maana taasisi zote zimeshachunguza kama TAKUKURU na nyinginezo
Maelekezo ya Lissu yanapitishwa na wabunge
Azimio la Saba: Kamati imethibitisha katibu mkuu wa wizara ya nishati na
madini amefanya uzembe pia amesaidia pesa za Escrow akaunti kulipwa kwa
asiyestahili, kamati inashauri uteuzi wake utenguliwe mara moja.
Waziri: Maswala yote yatachukuliwa hatua baada ya uchunguzi.
Kafulila: Halina mabadiliko na kama ni uchunguzi umeshafanywa na
CAG na TAKUKURU, bunge kama chombo kinachoisamamia serikali libaki na
meno yake ya kuisamamia serikali.
Simbachawene: Katibu mkuu ni mtumishi wa umma, na mwenye mamlaka nae ni raisi wa jamhuri hivyo bunge haliwezi.
Nagu: Nakubalianana uzito wa jambo, watendaji wa serikali
wanawajibika kweli lakini wana haki zao, mamlaka husika waangalie na
wachukue hatua.
Sendeka: Kamati inapendekeza uteuzi utenguliwe na TAKUKURU
wamfikisha mahakamani, sisi tumeshauri na watu ambao tuna mamlaka nao ni
waziri mkuu na raisi.
Zitto: Taarifa kwa waziri, taarifa hii inaweza kutumiwa na vyombo vya sheria.
Sakaya: Sio ikithibitika kwani kwa taarifa zilizopo imeshabitika
Suzan Lymo: Kwa uchunguzi ambao umeshafanyika, katibu mkuu huyu ana matatizo kwa sababu PAC na CAG ameshaonyesha
Vyombo vya kiuchunguzi viendelee kufanye uchunguzi
Lissu: Bunge litofautishe maswala la kijinai na mendine sio ya
kijinai kama kutengua uteuzi. Wapo wanaolindwa na sheria, lakini wapo
wanaoserve kwa mamlaka ya raisi hauwezi ukasema wana protection ya
kisheria. Tunaomba nipendekeze bunge linaazima na sio kupendekeza.
Zitto anapendekeza katibu mkuu asimamishwe kupisha uchunguzi.
Wasira: Lazima tukubali nchi inaendeshwa na mihimili mitatu, juzi
tulipata tatizo la mahakama kuzuia bunge na sisi pia bunge tusiingilie
serikali.
Mchangiaji: Uchunguzi utafanyikaje wakati watu wako kazini?
Werema: Mimi ndiye niliyemshauri Katibu Mkuu Maswi kushughulikia fedha, ninambeba hivyo shughulikeni na mimi
Imeshindikana kupita kwa azimio la saba, Spika kaamua waendelee na azimio la nane, watarudi kupiga kura mwishoni.
Azimio la nane: Bunge limemuondoa Naibu Waziri wa Nishati Masele kwenye mapendekezo kwa kuwa hana hatia ya kuadhibiwa
Azimio la tisa: Linajadiliwa kuhusu kutengua uteuzi wa Waziri Prof Muhongo lakini upande wa serikali imekataa
Bunge halina mamlaka ya kumwambia raisi atengue baada ya Lissu kulitaka bunge kutengua uwaziri wa Muhongo.
Mbaruku: Bunge kazi yake ni kushauri na bunge haliwezi kuwa messenger. (Anashauri anavyoona)
Muhongo ameshutumiwa amedanganya bunge lakini hamna popote iliposemwa
fedha hizi ni za umma moja kwa moja. Hivyo nashauri versin ya
muheshimiwa Chenge.
Shaha: Tunachohitaji ni lugha nzuri bila kudharau muhimili mwingine. Tuhoji na tumalize na tuulize wanaoafiki Lissu au Chenge.
Zitto: Akili yangu imechoka kidogo hivyo sina pendekezo.
Mbowe: Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo
kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani
yao. Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna
kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha
kulindana. Kwanini mnalinda wezi.
Baadhi ya wabunge wanasema wezi waondoke...
Sendeka: Naomba tukae na tujenge hoja, (Kelele zinaendelea)
SPIKA ANAAHIRISHA KIKAO CHA BUNGE MPAKA WASHAURIANE TENA(Spika aahirisha kikao cha Bunge ghafla baada ya kutokea sintofahamu baada ya Wapinzani kudai Waziri Muhongo analindwa )
0 comments:
Post a Comment