Tuesday, 18 November 2014
'Bikra' kigezo cha kuwa askari Indonesea
Serikali ya Indonesia inaelezwa kuruhusu
kuwafanyia wanawake wanaotaka kujiunga
na Jeshi la Polisi kipimo cha bikira ,shirika
la Human rights Watch limeeleza.
Shirika hilo uangalizi wa haki za binaadam
liliwahoji Polisi wanawake na wanaotaka
kujiunga na Jeshi la polisi ambao tayari
wamepimwa katika miji sita ya nchini
Indonesia,wawili kati yao wamefanyiwa kipimo
hicho mwaka huu.
Kipimo cha bikira kimeorodheshwa kuwa moja
ya matakwa ya kuingia kwenye Jeshi, tovuti ya
polisi imeeleza.
Wanawake waliofanyiwa kipimo hicho
wamesema walipata maumivu na kujisikia
kudhalilishwa.
Askari wa kike walishapeleka malalamiko kwa
ngazi za juu za jeshi la Polisi bila mafanikio.
Afisa wa juu wa Human Rights Watch,Nisha
Varia amesema kipimo hicho ni unyanyasaji na
kinawadhalilisha wanawake, amewataka polisi
mjini Jakarta kufuta kipimo hicho na kukipiga
marufuku nchi nzima.
Polisi nao wanasema kuwa hawafanyi kipimo
hicho kwa sasa kwa kuwa wamepiga marufuku.
Hata hivyo hakuna ushahidi wa kutosha kuwa
Jeshi la Polisi limesitisha kitendo hicho kwa
kuwa katika tovuti yake eneo la kazi tangazo la
tarehe 5 mwezi Novemba mwaka 2014
imeeleza kuwa wanawake wanaotaka kuwa
polisi wanapaswa kujaribiwa kama wana
bikira,hivyo basi wanawake wanaotaka kuwa
askari wanapaswa kutunza bikira
zao.
Wanawake walioolewa hawapewi nafasi
hiyo.
Mashuhuda wanasema kuwa jaribio la bikira
hufanywa katika hospitali zinazoendeshwa na
jeshi la Polisi, vidole hutumika katika kubaini
kama mwanamke ni bikira au la.
Shirika la Human Rights Watch limesema
kipimo hiki hufanywa na Polisi pia nchini
Misri, India na Afghanistan.
Mwaka 2010 Brigedia Jenerali, Sigit
Sudarmanto alieleza namna alivyotofautiana na
wenzake kuhusu kipimo cha bikira kwa
wanawake yeye haungi mkono.
Kisa cha kufanywa kwa kipimo hiki dhidi ya
wanawake ni madai kuwa hawahitaji wanawake
wasio bikira wakiwafananisha na makahaba.
Lakini swali linabaki kuwa je kuna ushahidi wa
kisayansi kuwa aliye bikira hufanya kazi kwa
ufanisi zaidi kuliko asiye bikira, je asiye na
bikira hana adabu kuliko aliye nayo?
Sudarmanto amesema baada ya kulumbana kwa
muda mrefu iliridhiwa kusitishwa kwa zoezi
hilo, hata hivyo inashangaza kuona bado hali ni
ileile japo ahadi ya kusitishwa ilitolewa.
Chanzo:BBC
0 comments:
Post a Comment