Matokeo ya awali ya mpango wa kulipa
wanawake ili kuwashawishi kunyonyesha
watoto umeonesha matokeo mazuri,
watafiti wameeleza.
Wakina mama katika maeneo matatu ya
Derbyshire,South Yorkshire nchini Uingereza ambapo kiwango
cha unyonyehsaji kiko chini kati ya asilimia 21
mpaka 29 waliahidiwa kulipwa mpaka pauni
200.
Kati ya wanawake 108 walio katika mpango
huu,wanawake 37 sawa na asilimia 34 tayari
wamelipwa katika kipindi cha wiki sita mpaka
nane.
Wakosoaji wakiwemo madaktari wanasema
mradi huu unachochea uwepo wa vitendo vya
rushwa.
Mpango mwingine utafuata ambao utakua
mkubwa zaidi utakaowahusisha wanawake
4,000
Tayari Wanawake 58 wamejiandikisha.
Nchini Uingereza, asilimia 51 ya wanawake kwa
kipindi cha wiki sita mpaka nane, scotland kwa
asilimia 38.
Takwimu ziko chini zaidi kwenye maeneo yaliyo
masikini mpka kwa kiasi cha asilimia 12.
Wataalamu wa afya wanasema watoto
wanatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama
pekee kwa kipindi cha miezi sita, ili kuwalinda
watoto dhidi ya maradhi.
Halikadhalika tafiti zinasema kuwa
kunyonyesha mtoto kunamuepusha mzazi
kupata maradhi ya saratani ya matiti na Ovari.
lakini hali haiko hivyo nchini Uingereza
ikilinganishwa na nchi nyingine, asilimia moja
tu ya watoto nchini humo hunyonya maziwa ya
mama zao kwa miezi sita.
Chanzo:BBC
0 comments:
Post a Comment