Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ameliagiza Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, kujenga daraja la muda linalounganisha wakazi wa mbagala kuu na kunduchi ambalo lilikatika kutoka na mvua.
Rais Kikwete ametoa agizo hilo wakati alipotembelea maeneo kadhaa yakiwamo ya Mbagala kuu na Jagwani ambayo yameathirika kutoka na mvua hizo zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam ambazo pia zimepeleka vifo vya watu 12 na wengine mamia kukosa makazi.
Aidha Rais Kikwete amewaagiza Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS
kupitia kwa mwakilishi wake Elisos Mtenga kusafisha mto msimbazi kwa
kuzoa taka zote na kuondoa mchanga uliojaa na kusababisha maji kushindwa
kupita.
Pia rais Kikwete ameahidi kuzungumzia hali ya mafuriko yaliyotokea katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam kesho baada ya kuhitimisha ziara ya kutembelea maeneo hayo.
Pia rais Kikwete ameahidi kuzungumzia hali ya mafuriko yaliyotokea katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam kesho baada ya kuhitimisha ziara ya kutembelea maeneo hayo.
0 comments:
Post a Comment