Vyama vya Upinzani nchini Burundi vimeiomba serikali ya Tanzania kumshinikiza rais Pierre Nkurunziza aachane na mpango wake wa kugombea urais wa nchi hiyo kwa awamu ya tatu, kwani hatua hiyo sio tu ni kinyume na katiba ya Burundi, bali ni hatari kwa usalama wa eneo zima la maziwa makuu.
Kiongozi wa vuguvugu la maandamano ya upinzani
yanayoendelea nchini Burundi hivi sasa Bw. Mugwengezo Chauvineau,
amesema hatua hiyo ya rais Nkurunziza italeta matatizo makubwa ambayo tayari yameshaanza kuonekana kupitia maelfu ya wakimbizi wanaoingia katika nchi hizo.
Bw. Chauvineau amewataka washiriki wa mkutano wa Burundi utakaofanyika
jijini Dar es Salaam kesho kutumia fursa hiyo kuiokoa Burundi kwani hali
ya usalama nchini humo hivi sasa sio nzuri kutokanana na kuzagaa kwa
silaha ambazo zinaweza kuvuka na kuhatarisha amani katika nchi zote
zilizopakana na Burundi.
0 comments:
Post a Comment