Facebook

Thursday, 3 July 2014

Ajali ya ndege yawaua watu wanne Kenya

Ajali ya ndege Nairobi
Shughuli za uokozi zikiendelea baada ya ndege ya mizigo kuanguka jijini Nairobi
Watu wanne akiwemo Rubani wa ndege moja ya mizigo, wamefariki dunia baada ya ndege walimokuwa kuanguka mapema leo asubuhi katika mtaa wa Embakasi jijini Nairobi.
Kwa mjibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, ndege hiyo ilianguka dakika chache tu baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba shehena ya Miraa ama Mairungi kuelekea Mogadishu nchini Somalia.
Uchunguzi umeonyesha kuwa ndege hiyo huenda iligonga mlingoti wa stima karibu na mtaa wa Embakasi, mjini Nairobi na kuanguka.

Related Posts:

  • Mama anayeugua Ebola atoroshwa Mwanamke aliyeambukizwa Ebola atoroshwa Hospitalini huko Freetown Hali ya Tahadhari imetangazwa mjini Freetown Sierra Leone baada ya mwanamke mmoja aliyeambukizwa Ebola kutoroshwa kutoka Hospitalini na jamaa zake kw… Read More
  • Juhudi za kutafuta amani Gaza zaingia dosari. Wapalestina zaidi ya 800 wameuawa na Waisraeli 35 Israeli imeendelea kuivirumishia makombora Gaza kucha kutwa ,huku kikao cha mawaziri wa baraza la Usalama kikitarajiwa huko Marekani kujadili mapendekezo mapya ya … Read More
  • Mabaki ya ndege Algeria yaonekana Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali. Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeang… Read More
  • Maandamano yazuka Palestina polisi wakabiliana na raia Palestina Maandamano makubwa yamefanyika katika ukingo wa Magharibi mwa Palestina karibu na mpaka wake na Israel kupinga mashambulio yanayofanywa na Israel. Waandamanaji hao wakiwa na hasi… Read More
  • Air Algerie AH5017: Abiria wote waliaga Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani Abiria wote na wahudumu wa ndege ya Air Algerie AH5017 waliangamia jangwani. Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi … Read More

0 comments:

Post a Comment