Bolivia
imeteremsha umri halali wa kufanya kazi ili kuruhusu watoto kufanya
kazi kuanzia umri wa miaka 10 kwa masharti kuwa lazima waendelee kwenda
shule na wawe wamejiajiri.
Sheria hiyo pia inaruhusu watoto wenye umri wa miaka 12 kuajiriwa, lakini watahitaji ruhusa kutoka kwa wazazi wao.
Makamu wa rais Alvaro Garcia Linera amesema sheria hiyo mpya inaakisi mahitaji ya Bolivia, moja ya nchi masikini zaidi Amerika ya Kusini.
Sheria hiyo pia inajumuisha adhabu kali kwa watu watakaonyanyasa watoto ikiwa ni pamoja na adhabu ya miaka 30 kwa kosa la mauaji ya mtoto.
Hatua hiyo iliidhinishwa na bunge la Congress mapema mwezi huu, na kutiwa saini na Bwana Garcia, kwa kuwa Rais Evo Morales ambaye yuko ziarani nchini Brazil.

0 comments:
Post a Comment