Facebook

Sunday, 20 July 2014

Waasi watuhumiwa "Kuharibu uushahidi" baada ya kuanguka ndege ya Malaysia

 Salim Kikeke's photo.

Ukraine imetuhumu waasi wanaoiunga mkono Urusi kwa kujaribu kuharibu ushahidi wa "uhalifu wa kimataifa" katika eneo ndege ya Malaysia ilipoanguka.
Serikali imesema waasi wakiongozwa na Urusi wanazuia wawakikishi wa kimataifa na wataalam wake kuzuia uchunguzi.
Inaaminika ndege hiyo namba MH17 ilianguka baada ya kudunguliwa na kombora, katika eneo linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa Ukraine siku ya Alhamisi.
Watu wote 298 waliokuwemo ndani walipoteza maisha.
Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilikuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur. Ilianguka kati ya Krasni Luch katika eneo la Lihansk na Shakhtarsk karibu na Donetsk. 

Salim Kikeke's photo. Katika taarifa yake, serikali ya Ukraine imelalamika kwa kusema "magaidi" wamechukua miili 38 na kuipeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika eneo linalodhibitiwa na waasi katika jiji la Donetsk. Imesema pia waasi wanajaribu kusafirisha mabaki ya ndege kwenda Urusi.

0 comments:

Post a Comment