Christian Gourcuff ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Algeria siku ya Jumamosi. Raia huyo wa Ufaransa anachukua nafasi ya Vahid Halilhodzic aliyewapeleka Mbweha wa Jangwani katika raundi ya pili ya Kombe la Dunia Brazil.
Gourcuff kwa muda mrefu alitajwa kuchukua nafasi hiyo baada ya michuano ya Brazil, lakini habari hizo zimethibitishwa baada ya kukutana na shirikisho la soka la Algeria.
Shirikisho hilo limesema Gourcuff, 59, ataanza kazi Agosti 1.
Amepewa mkataba hadi mwisho wa Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Kazi yake ya kwanza itakuwa dhidi ya Ethiopia mwezi Septemba katika mechi za kufuzu kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika.
0 comments:
Post a Comment