Hatahivyo Robben mwenye miaka 30 aliomba msamaha katika vyombo vya habari mara baada mechi kumalizika kwa ushindi wa 2-1 huku goli la ushindi likifungwa mara baada ya mwamuzi wa mechi hiyo kutoa adhabu ya penati huku akidhani Robben alikuwa amefanyiwa madhambi katika eneo la penati na beki wa Mexico Rafael Marquez.
Pinto ambaye ndio kocha mkuu wa Costa Rica alisikika akisema kuwa, amewaomba Fifa pamoja na mwamuzi wa mechi yao hiyo ya Jumamosi kumtupia jicho la ziada winga huyo ili asije akaigharimu timu yao katika kuelekea kwenye nusu fainali ya michuano hii ya Kombe la Dunia.
Costa Rica imefikia katika hatua ya robo fainali mara baada ya kuiondoa Ugiriki katika changamoto ya mikwajuu ya penati.
Mechi hiyo ya leo Jumamosi inatazamiwa kuanza saa 5 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa Arena Fonte Nova uliopo katika Jiji la Salvador
0 comments:
Post a Comment