

Real Madrid wana uhakika wa kumsajili kwa pauni milioni 30 kipa wa Manchester United, David De Gea, 24, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake (Sun)

De Gea tayari amewaaga wachezaji wenzake wa Man United (Daily Star), Manchester City wanamtaka kiungo wa Real Madrid Isco, 23, ili kuchukua nafasi ya David Silva, 29 (Daily Mirror),

Chelsea wanapanga kutoa pauni milioni 30 kumchukua mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain ambaye amehusishwa na kuhamia Arsenal, Liverpool na Manchester United (Daily Star),
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ametupilia mbali tetesi kuwa Diego Costa, 26 anataka kurejea Spain (Sun),
Chelsea na Manchester United wanamgombea beki wa kati wa Atletico Madrid Joao Miranda, 30, ambaye mkataba wake unaisha msimu ujao (Daily Telegraph),

kipa wa Ufaransa na Tottenham Hugo Lloris, 28, hajakanusha kuwa anataka kuondoka White Hart Lane (Guardian).
0 comments:
Post a Comment