Waziri mkuu wa zamani wa Italy, Silvio Berlusconi, ameshinda rufaa yake dhidi ya mashtaka ya kulipa kufanya mapenzi na kahaba mwenye umri mdogo.
Majaji katika mahakama ya Milan wametupilia mbali hukumu iliyotolewa
na mahakama ya chini mwaka jana, kuwa alilipa fedha kwa mcheza dansi
anayejulikana kama Ruby, mwenye umri wa miaka 17.
Msichana huyo
amekanusha tuhuma za ukahaba. Rufaa hii inamaanisha kifungo cha miaka
saba jela na amri ya kutojihusisha na siasa, sasa vimetupiliwa mbali.
Waendesha mashtaka wana haki ya kupinga uamuzi huu katika mahakama ya
juu zaidi.
0 comments:
Post a Comment