Facebook

Saturday, 19 July 2014

UEFA YABADILI SHERIA YA KADI, KUNUSURU WACHEZAJI KUKOSA FAINALI!

UEFA Champions League
JOPO LA DHARURA LA UEFA limetangaza mabadiliko ya Sheria ya Malimbikizo ya Kadi za Njano kumalizikia hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Klabu Barani Ulaya ili kunusuru Wachezaji kutokosa Fainali.

Uamuzi huu utanusuru yale yaliyomkuta Kiungo wa Real Madrid Xabi Alonso Msimu uliopita wakati alipolimbikiza Kadi za Njano Tatu tangu hatua za awali na ya mwisho kupewa kwenye Nusu Fainali na Bayern Munich na hivyo kufungiwa Mechi moja na kuikosa Fainali Real waliyoifunga Atletico Madrid 4-1.

Sheria ya Malimbikizo ya Kadi za Njano Tatu kumalizikia hatua ya Robo Fainali ilikuwepo kwenye Mechi za Mataifa ya Ulaya lakini kwa Klabu haikuwepo na sasa kuanzia Msimu ujao Mashindano ya Klabu, Ligi Mabingwa barani Ulaya na EUROPA, yatatumia Mfumo huu mpya.

Hivyo, Kadi za Njano zote kuanzia hatua ya Makundi zitafutwa baada ya Robo Fainali na kuanzia Nusu Fainali kila Mchezaji atahesabika hana Kadi.
UEFA wametamka kuwa wameamua kuchukua uamuzi huu kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ya Klabu na kupitishwa na Jopo la Dharura la UEFA kuanza kutumika mara moja.
Bila shaka uamuzi huu utapokewa vyema na Wadau wengi ambao huchukizwa kuona Mastaa wao wakikosa Mechi muhimu ya Fainali.

0 comments:

Post a Comment