Brazil imemtangaza mchezaji wa zamani Dunga kuwa kocha wa timu ya
taifa, kwa mara ya pili.
Dunga alikuwa nahodha wa Brazil mwaka 1994
waliposhinda Kombe la Dunia, na alikuwa kocha kuanzia mwaka 2006 hadi
2011.
"Nimefurahi sana kurudi," amesema Dunga, 50, ambaye alikuwa akitajwa sana kuchukua nafasi hiyo.
Dunga anachukua nafasi ya Luiz Filipe Scolari, aliyejiuzulu baada ya
Brazil kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014, lakini alipata kipigo
kizito katika historia ya taifa hilo kwa kufungwa 7-1 na Ujerumani.
Dunga aliifikisha Brazil katika robo fainali Afrika Kusini mwaka 2010.
Imeandaliwa na.....
Katemi P.Methsela (Blogger)
Imeandaliwa na.....
Katemi P.Methsela (Blogger)
Endelea kutembelea www.bantutz.com kupata habari mbalimbali kutoka katika kila pande ya dunia kwa muda na wakati muafaka.Jukumu letu sisi ni kukuhabarisha,hatutasita kukufikishia kila kitakachokuwa kimetufikia.
0 comments:
Post a Comment