Filamu yenye utata kuhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Nigeria
katika miaka ya 1960, itaanza kuoneshwa katika majumba ya sinema kuanzia
mwezi Agosti, baada ya wadhibiti filamu kuruhusu ioneshwe.
Filamu hiyo- Half of a Yellow Sun, inayohusu vita vya Biafra ilikuwa
ianze kuoneshwa mwezi Aprili, lakini bodi ya filamu nchini humo ilisema
baadhi ya vipande katika filamu hiyo vilikuwa havikubaliki.
Filamu hiyo
imetengenezwa kutokana na kitabu kilichoandikwa na mwandishi maarufu wa
vitabu Chimamanda Ngozi Adichie. Zaidi ya watu milioni moja walikufa
katika vita hivyo, vilivyosababishwa na jaribio la kujitenga la majimbo
ya kusini mashariki ya Nigeria. Kulikuwa na wasiwasi kuwa filamu hiyo
huenda ingeleta mvutano wa kikabila.
0 comments:
Post a Comment