Rapa Jay Z ameingia katika mapambano na mtayarishaji muziki Chauncey Mahan kutokana na kitendo cha jamaa huyu kuibuka na rekodi za rapa huyu alizozifanya kati ya mwaka 1998 na 2002, na kujaribu kumuuzia kwa dola laki 1 za kimarekani, mpango ambao tayari umeingiliwa na polisi kutafuta suluhu yake.
Rekodi hizi za Jay Z zinakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 15 mpaka 20, na kwa mujibu wa taarifa, Jay Z pamoja na timu yake walikuwa wakifahamu kuwa zimekwishapotea, mpaka pale Chauncey Mahan alipoamua kuibuka nazo na kudai gharama za kuzihifadhi kwa muda wote ambao zilikuwa chini yake.
Katika jaribio la mtayarishaji huyu kukutana na wawakilishi wa Jay Z kwaajili ya kufanya bishara ya rekodi hizi, mtayarishaji muziki huyu alijikuta chini ya ulinzi na kulazimika kuwapatia nakala ya rekodi hizo polisi huku uchunguzi dhidi yake ukiendelea
Endelea kutembela katemimethsela.blogspot.com kujua kitakachojiri juu ya bifu hili
0 comments:
Post a Comment