Israel imeonya maelfu ya Wapalestina mashariki na kaskazini mwa Gaza na kuwataka kuondoka majumbani mwao huku ikiendelea na mashambulizi ya anga.
Onyo hilo linakuja baada ya mpango wa kusitisha mapigano wa Misri kugonga mwamba.
Hamas awali ilitupilia mbali makubaliano hayo, lakini baadaye afisa mmoja amesema kuwa watafikiria suluhu ya kisiasa.
Maafisa wa Palestina wanasema mashambulio ya Israel yamesababisha vifo vya watu 204 mpaka sasa. Israel, siku ya Jumanne iliripoti kuuawa kwa mtu mmoja.
Watu kumi waliripotiwa kufa Gaza katika mashambulio ya usiku.
Kurejea kwa mashambulio ya anga kumekuja baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kusema "hana jinsi" ila kufanya harakati za kijeshi.
0 comments:
Post a Comment