Facebook

Thursday, 17 July 2014

TUFANI LAZUA TAFRANI UFILIPINO

 Salim Kikeke's photo.

Upepo mkali umesababisha umeme kukatika na kulazimisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao kufuatia Tufani Rammasun kugonga visiwa vya Ufilipino.
Tufani hilo ambalo pia linajulikana kama Glenda, liligonga kisiwa kikuu cha Luzon likiwa na upepo wenye kasi ya kilomita 185 kwa saa.

Salim Kikeke's photo. Mamlaka zinasema watu wasiopungua wanne wamekufa kutokana na kimbunga hicho.
Maafisa wanasema kiini cha kimbunga hicho kimuepita mji mkuu, Manila, lakini hali mbaya ya hewa ilisababisha shughuli zote kusimama.

Salim Kikeke's photo. Ofisi za serikali na shule zilifungwa siku ya Jumatano, huku safari za ndege zikifutwa.
Zaidi ya watu 370,000 wengi kutoka jimbo la mashariki la Albay ambalo liliathirika kwanza na tufani, wamehamishwa, limesema shirika la Msalaba Mwekundu.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment