Facebook

Saturday, 5 July 2014

Kocha wa Ujerumani akisifia kikosi chake

Kocha wa Ujerumani Joachim Low amekimwagia sifa kikosi chake mara baada ya kuifungisha virago timu ya Ufaransa katika mchezo wa robo fainaili kwa ushindi wa goli 1-0.
Low amesema kuwa mbinu za kiuchezaji walizonazo wachezaji wake zinaweza kuwafikisha katika hatua ya fainali katika michuano hii ya Kombe la Dunia, hata hivyo aliendelea kusisitiza kuwa bado timu za taifa za Marekani ya Kusini zina nafasi kubwa ya kulichukua Kombe hilo la Dunia.
Kocha huyu pia aliwamwagia sifa walinzi wa timu zote mbili kwani kulikuwa hakuna nafasi nyingi za kufunga zilizotengenezwa, pia aliwasifia walinzi wake kwakufanikiwa kumbana mbavu Karim Benzema asipate mwanya wa kuwaumiza.
Alisema kuwa kabla ya mchezo nilipitia kikosi cha Ufaransa nikagundua wana wachezaji wazuri katika nafasi ya kiungo mkabaji, ambako Cabaye na Pogba wamekuwa katika kiwango bora katika michuano hii wakicheza kwenye nafasi hiyo ndio maana ni kafanya maamuzi ya kumtoa Philip Lahm katikati na kumchezesha akitokea pembeni, huku Jerome Boateng akirudi katika nafasi ya beki wa katikati nafasi iyokuwa imeachwa wazi na beki Per Mertesacker.
Hatahivyo maamuzi hayo yaliweza kuzaa matunda.
Japokuwa beki Matt Hummels alitangazwa kama mchezaji bora wa mechi lakini naamini hata mlinda mlango wetu Manuel Neuer ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani kwani aliweza kuokoa michomo mingi ya wazi katika dakika za majeruhi za mchezo, alisikika kocha huyo wa Ujerumani akisema.
Ujerumani itakutana na Brazil katika hatua ya nusu fainali mara baada ya kuifunga Colombia kwa bao 2-1.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment