Libya imelionya baraza la
usalama la umoja wa mataifa kwamba iwapo haitapata usaidizi wa
kuimarisha vikosi vyake vya usalama taifa hilo litakuwa miongoni mwa
mataifa yaliofeli.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Libya
Mohammed Abdelaziz ameliambia baraza hilo kwamba taifa lake linahitaji
wataalam kuwafunza maafisa wa polisi na wanajeshi ili kulinda miundo
mbinu muhimu kama vile visima vya mafuta,bandari na viwanja vya ndege.Ameliagiza baraza hilo kuchukua hatua za haraka iwezekanavyo.
kumekuwa na ongezeko la visa vya ghasia kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo nchini Libya na tayari umoja wa mataifa umewaondoa maafisa wake wa kimataifa kutoka taifa hilo.
0 comments:
Post a Comment