Facebook

Saturday, 19 July 2014

TUANGAZIE VITIMBI NA VIHOJA LIGI YA KAGASHEKI



Ligi ya soka ya  kagasheki cup leo 19/07/214 l mzunguko wa kwanza umemalizika katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Huku ikilalamikiwa na wadau mbali mbali wa mchezo huo wenye mashabiki lukuki Duniani. 

 Wakiongea na BantuTz kwa nyakati tofauti wamedai ni jambo la kushangaza kwa Chama Cha Mpira cha Manispaa kuruhusu ligi kuanza bila zawadi kujulikana, pia wamelaani vitendo vya rushwa katika soka na vile vya upangaji matokeo kwa baadhi ya timu.
Ligi hiyo inayodhaminiwa na mbunge wa jimbo la Bukoba mjini mh Balozi Khamis Kagasheki, aliyewahi kuwa waziri wa Maliasili na Utalii.
 
Nao wafatiliaji wa maswala ya soka wamehoji kuwa kama mbunge atasimamia ahadi yake ya kuwa ataongeza zawadi kila mwaka basi ligi ya mwaka huu itakuwa na zawadi ya zaidi ya milioni saba kwa mshindi wa kwanza.

Timu nyingi zinazo shiriki ligi hiyo zinasadikika kununua wachezaji nje ya Manisipaa ya Bukoba na nje ya mkoa wa kagera, kitendo icho sio cha kuinua soka kwa mkoa na kwa Bukoba kwa ujumla. Wafatiliaji wa maswala ya soka mkoani hapa wanasema michezo inashuka kwa sababu ya siasa kuingilia mambo ya msingi.
 
Waamuzi wa ligi hiyo wamepongezwa kwa kujitahidi kufanya maamzi makini katika mzunguko wa kwanza ingawa makosa yalikuwepo, pia baadhi ya mashabiki wamesema usalama uimariswe zaidi kwani sehemu za mikusanyiko kama hizi watu wasiopenda amani na maendeleo wanaweza kutumia mwanya huo.
 
Jumla ya kata zote 14 za jimbo la Bukoba mjini zimeshiriki ligi hiyo ya Kagasheki cup 2014/ 2015, ubingwa wa ligi hiyo unashikiliwa na kata ya bilele.   

Kata zilizo shiriki ni KASHAI, BILELE, HAMUGEMBE, KIBETA, IJUGANYONDO, KITENDAGULO, RWAMISHENYE, BAKOBA, BUHEMBE, MIEMBENI, KAGONDO, KAHORORO, NSHAMBYA NA NYAHANGA.

 

Imeandaliwa na....
                              Katemi P,Methsela
                              (+255 785 442 107) 

                              Venance Victoria Magege.
                               (+255 715 904 910)
 

0 comments:

Post a Comment