Facebook

Sunday, 13 July 2014

LIVERPOOL NA BARCA WAKUBALIANA JUU YA SUAREZ

 Photo: LIVERPOOL NA BARCA WAKUBALIANA JUU YA SUAREZ
Liverpool wamefikia makubaliano ya kumuuza Luis Suarez kwenda Barcelona. Ada ya uhamisho inadhaniwa kuwa takriban pauni milioni 75.
Suarez alijiunga na Liverpool mwaka 2011 akitokea Ajax, kwa pauni milioni 22.7. Alikuwa amesalia na miaka minne katika mkataba wake uliokuwepo na Liverpool. Alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa England, baada ya kupachika mabao 31 ya ligi msimu uliopita.
Suarez kwa sasa anatumikia adhabu ya miezi minne na mechi tisa za kimataifa kwa kumng'ata Giorgio Chiellini wa Italy wakati wa mechi ya Kombe la Dunia Brazil.

Related Posts:

  • ADHABU YA POWELL YAPUNGUZWA    Bingwa wa zamani wa mbio za mita 100 Asafa Powell na Sherone Simpson wote kutoka Jamaica wamepunguziwa adhabu ya kufungiwa, kutoka miezi 18 hadi miezi sita. Uamuzi uliotolewa na mahakama ya usuluhisi wa m… Read More
  • Adebayor augua Malaria,atakosa ziara za Marekani.   Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Emmanuel Adebayor atakosa ziara ya Marekani baada ya kuukutwa na Malaria. Adebayor, 30, alilazwa hospitali siku ya Jumamosi kwa kile klabu yake imesema "homa ndogo" ya malaria. A… Read More
  • Adidas waingia mkataba mnono na Manchester United.    Kampuni ya Adidas imesaini mkataba wa pauni milioni 750 wa kutengeneza jezi za Manchester United kwa miaka kumi kuanzia msimu ujao. Hatua hii imekuja baada ya mahasimu wao wa Marekani, Nike, kuamua kutoen… Read More
  • Ujeruman yapokelewa kwa shangwe.   Maelfu ya mashabiki wa soka nchini Ujerumani wamejitokeza mjini Berlin kuwalaki wachezaji wa timu ya taifa walioshinda Kombe la Dunia. Sherehe kubwa zimefanyika katika eneo la Brandenburg Gate, ambapo wacheza… Read More
  • MATOKEO YAZUA VURUGU ARGENTINA   Polisi wa Argentina wamepambana na waandamanaji katika mji mkuu, Buenos Aires baada ya nchi hiyo kufungwa na Ujerumani katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia. Mapema jana jioni maelfu ya watu walikusanyika… Read More

0 comments:

Post a Comment