Meneja
wa Liverpool Brendan Rodgers ataruhusiwa kutumia fedha zote, pauni
milioni 75 za mauzo ya Luis Suarez kuimarisha kikosi chake (The
Times),
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anayetafuta kiungo mkabaji
anapanga kuwachukua Sami Khedira, 27, na Lars Bender, 25 (Daily
Telegraph),
Hata hivyo Chelsea wapo tayari "kuuteka" mchakato wa Sami
Khedira na kumsajili mchezaji huyo wa Real Madrid (Daily Mirror),
Crystal Palace wanakaribia kumsajili Fraizer Campbell kutoka Cardiff
City (Guardian),
Newcastle wanakaribia kumsajili Emmanuel Riviere, 24,
kutoka Monaco, mchezaji huyo amehusishwa pia na kwenda Arsenal, Stoke
City na West Brom (Evening Chronicle)
Arsenal na Tottenham wanamwania
Loic Remy, 27, ingawa Newcastle huenda wakafanikiwa kumsajili mchezaji
huyo wa QPR aliyecheza msimu uliopita kwa mkopo (Talksport),
Stoke wako
karibu kumsajili Bojan Krkic, 23, kutoka Barcelona (Daily Star),
Inter
Milan wanafikiria kumsajili beki kutoka Chile Gary Medel, 26 anayechezea
Cardiff (Sky Sports),
Manchester United na Chelsea wanamgombea kiungo
Alex Song, 26, na Barcelona wako tayari kupokea pauni milioni 20 (Daily
Star),
Newcastle wamekubaliana na Montpellier kumsajili kiungo
mshambuliaji Remy Cabella, 24 (Daily Express),
West Ham wamepata
upinzani kutoka Sevilla na AC Milan kumsajili mshambuliaji wa Ecuador
Enner Valencia anayechezea Pachuca ya Mexico (Times),
Chelsea
wanafikiria kutoa dau la pauni milioni 7 kumchukua kiungo Adrien Rabiot,
19, kutoka Paris St-Germain (Daily Express),
Real Madrid wanafikiria
kumchukua mshambuliaji wa Manchester United Danny Welbeck kuziba nafasi
ya Alvaro Morata anayetarajia kujiunga na Juventus (Daily Star),
Arsenal
tayari wametangaza dau la euro milioni 25 kwa Sami Khedira, ingawa
Chelsea nao wanamtaka kiungo huyo wa Real Madrid (Daily Express),
Bebe, 23,
anataka kuhamia Benfica kwa uhamisho wa kudumu. Bebe alikuwa kwa mkopo
Pacos Ferreira ya Ureno (A Bola),
Arsenal wanakaribia kumsajili beki wa
kulia Javi Manquillo kwa mkopo kutoka Atlètico Madrid (Daily Telegraph),
Tottenham wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 18 kumsajili
mshambuliaji wa Swansea Wilfried Bony (Daily Star).
Share tetesi hizi na
wapenda soka wote. Tetesi nyingine kwenye magazeti na mitandao ya
Jumapili tukijaaliwa. Cheers!
0 comments:
Post a Comment