Facebook

Tuesday, 8 July 2014

Nguli wa Real Madrid afariki dunia.

 Photo: MKONGWE WA REAL MADRID AFARIKI DUNIA
Mchezaji nguli wa Real Madrid Alfredo Di Stefano, anayetajwa kuwa mmoja wa wachezaji wazuri duniani amefariki dunia.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid aliyekuwa na umri wa miaka 88 alipatwa na mshtuko wa moyo siku ya Jumamosi na kulazwa katika hospitali ya Gregorio Maranon mjini Madrid.
Real Madrid imethibitisha taarifa hizo, ikisema Di Stefano ambaye ni Rais wao wa heshima amefariki dunia.
Katika uhai wake alishinda makombe matano ya Ulaya, akifunga katika kila mchezo wa fainali kati ya mwaka 1956 na 1960.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amesema bodi ya klabu 'imesikitishwa na kupeleka rambirambi kwa watoto, familia na marafiki'.
Alizaliwa nchini Argentina, lakini mafanikio yake aliyapata Ulaya kwa kuweza kushinda vikombe vinane vya ligi kuu ya Spain, na kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya mwaka 1957 na 1959.

Related Posts:

  • John Stones nje hadi 2015 Beki wa Everton na timu ya taifa ya England John Stones huenda asicheze hadi mwakani baada ya kuthibitishwa kuwa anahitaji kufanyiwa upasuaji katika kifundo cha mguu. Stones, 20, aliumia katika mchezo dhidi ya Mancheste… Read More
  • Ratiba Ligi Kuu Uingereza RATIBA | England - Premier League Kesho Jumamosi 17:00 Hull City vs Crystal Palace 17:00 Leicester City vs Burnley 17:00 Liverpool vs West Bromwich Albion 17:00 Sunderland vs Stoke City 17:00 Swansea City vs Newcastle Uni… Read More
  • Ronaldo kuzeekea Real Madrid   Cristiano Ronaldo hana nia ya kurejea Manchester United na atamalizia kucheza soka yake Real Madrid, amedai wakala wake Jorge Mandes.  Ronaldo, 29, tayari amefunga magoli 15 msimu huu, ikiwemo kufikisha … Read More
  • Daley Blind "Siko tayari kulinganishwa na Roy Keane"  Blind alisema ameyazoea maisha ya Manchester United kwa muda mfupi,lakini asisitiza kuwa nimapema sana kumlinganisha na Roy Kean, Blind alisema "tusiende mbali sana,maendeleo yangu ni mazuri kwa sasa lakini ndo kwanz… Read More
  • RATIBA YA MECHI LIGI KUU YA UINGEREZA .BantuTz SPORTS RATIBA YA MECHI LIGI KUU YA UINGEREZA LEO HII 14:45 Liverpool vs Everton 17:00 Chelsea vs Aston Villa 17:00 Crystal Palace vs Leicester City 17:00 Hull City vs Manchester City 17:00 Manchester United vs West… Read More

0 comments:

Post a Comment