Aliendelea kusema kuwa kikosi chao cha Uholanzi ndio kilistahili na ushindi hapo jana, kwa sababu walitengeneza nafasi nyingi zaidi ya kikosi kilichokuwa kinaongozwa na Lionel Messi.
Robben alisema kuwa, “ninao uhakika katika mechi ya fainali Ujerumani italinyakuwa kombe hilo kwa sababu kikosi chao ni bora zaidi ya kikosi cha Argentina.”
Wakati huo huo kiungo huyo wa Uholanzi alisikika akisema kuwa wapinzani wao walikuwa wakilinda lango muda wote, na kwamba walikuwa wakipoteza muda kwa kupigiana pasi zisizokuwa na malengo ili mradi muda wa kupigiana mikwaju ya penati ufike mapema.
Katika mechi hiyo ya nusu fainali Uholanzi walifungwa na Argentina kwa changamoto ya mikwaju ya penati 2-4, ambapo beki wa Uholanzi Vlaar pamoja na kiungo wao Sneijder walishuhudia penati zao zikiokolewa kwa umahiri na kipa wa Argentina Sergio Romero.
Hivyo Argentina watapambana Ujerumani katika mechi ya fainali iakayochezwa July 13 katika uwanja wa Maracana mjini Rio De Janeiro.
0 comments:
Post a Comment