Zaidi ya mashabiki mia mbili wa soka kutoka Ghana walioingia Brazil
kwenda kutazama Kombe la Dunia wameomba hifadhi ya ukimbizi nchini humo.
Polisi wa Brazil katika mji wa Caxias do Sul wamesema mashabiki
hao wamewaambia kuwa wanakimbia mizozo baina ya makundi ya Kiislam
nchini mwao.
Wizara ya sheria bado haijafikia uamuzi wowote kuhusu
maombi hayo ya ukimbizi - kuyakubali au la.
Baadhi yao inadaiwa wanaishi
katika kituo kimoja cha Kanisa Katoliki kinachotoa misaada kwa
wahamiaji.
Ghana ilimaliza katika nafasi ya mwisho katika kundi lao,
baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Marekani na Ureno na kutoka sare na
Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment