Baadhi ya tetesi za usajili katika ligi mbali mbali barani ulaya msimu wa 2014/2015
Straiker wa klabu ya Galatasaray ya Uturuki Didier Drogba 36, yupo
katika mazungumzo na klabu yake ya zamani Chelsea juu ya uwezekano
wakurudi Stamford Bridge kwa mkataba wa mwaka mmoja, kiiStaa huyo
aliondoka katika timu hiyo mwaka 2012 baada ya kuisaidia timu hiyo
kunyakuwa ubingwa wa Uefa Champions League kwa mara ya kwanza baada ya
kuifunga Buyern munich katika changamoto ya mikwaju ya penati, pia
amewahi kupata vikombe vitatu vya premier league, FA cup mara nne,
pamoja na League Cup mara mbili
Mlinzi wa kati Dejan Lovren 25, wa klabu ya
Southampton anajianda kujiunga na klabu ya Liverpool baada ya vilabu
hivyo kukubaliana ada ya uhamisho ya pauni milioni 20, Deal hilo
linatazamiwa kukamilika ndani ya wiki hii, hiyo ni kwa mujibu wa gazeti
la Times la nchini Uingereza
Klabu ya soka nchini Ujerumani Buyern
Munich inajianda kukibomoa tena kikosi cha Borrusia Dortmund kwa kufanya
usajili wa Marco Reus 25, kwa ada ya euro milioni 35 ambazo zipo katika
kipengele cha mkataba wa mchezaji huyo pamoja na klabu yake. Tayari
Buyern Munich wameshafanya usajili wa Mario Gotze na Robert Lewandowisk
wote kutoka klabu ya Borrusia Dortmund
Man United wanajianda kutuma ofa nyingine
kwa klabu ya Juventus juu ya uhamisho wa kiungo wao Arturo Vidal 27,
kwa ada inayokadiriwa kuwa euro milioni 54
Klabu ya Ac Milani ya Italia imefungua
milango kwa timu yoyote itakayo hitaji kumsajili Straiker wao mtukutu
Mario Balloteli 24, kwa ada ya euro milioni 20, hapo awali klabu ya
Arsenal iliripotiwa kumhijati mchezaji huyo lakini taarifa za hivi punde
zinadai kuwa kocha wa Klabu hiyo Arsene Wenger kwasasa hivi hana mpango
wa kusajili mshambuliaji mara baada ya ujio wa Alexis Sanchez kutoka
katika klabu ya Barcelona
0 comments:
Post a Comment