Viungo mbali mbali vya binadamu vimekutwa katika eneo
la kutupa taka la Bunju mjini Dar es Salaam katika mazingira ambayo
haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka wapi.
Kwa mjibu wa Afisa mmoja wa polisi ambaye
hakutaka jina lake litajwe amesema viungo hivyo vya binadamu
vilivyokutwa ni miguu,vidole ambavyo vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani
ya mifuko.Mtu mmoja anashikiliwa kuhusishwa na tukio hilo ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo vya binadamu.
Haijafahamika mara moja miili hiyo ya binadamu imetolewa wapi na ilipelekwa eneo hilo kwa lengo gani.
Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino ambapo viungo vyao huchukuliwa,japo kuwa viungo hivi vilivyokutwa kwa sasa bado havihusishwi moja kwa moja na matukio ya mashambulizi na mauaji ya walemavu hao.
Mpaka tunaondoka eneo la Tukio Miili
ilikuwa imechukuliwa na Jeshi la Polisi kwa Uchunguzi zaidi, Taarifa
kamili italetwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam.Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino ambapo viungo vyao huchukuliwa,japo kuwa viungo hivi vilivyokutwa kwa sasa bado havihusishwi moja kwa moja na matukio ya mashambulizi na mauaji ya walemavu hao.
Nukuu ya mwanafunzi wa IMTU.
"For a while our university administration imekua na matatizo.Iliwahi kutokea miaka ya nyuma scenario kama hiyo ambapo mwanafunzi alieonekana na mkono mtaani of which hairuhusiwi hata kutoka na groves nje ya hicho chumba..
Sasa semester one ilimaliza kutumia hizo dead body on march zikatakiwa zitupwe..
kwa kuwa kifaa kilikua kibovu waliomba MuHAS wawasaidie ambapo inasemekana walisema nao kifaa(according to the guy anayehusika) Chuo Chao kina shida wakaomba hindu mandal wakatakiwa kutoa 7m..ikacheleweshwa kutolewa..
Leo umoja wa vyuo vya madaktari Afrika mashariki ulikuja for inspection kwakua hazikutakiwa kuonekana wakaamua kufanya hivyo of which is illegal..
On friday nilikua mwenyewe ofisini and i heard one of teachers anaongelea kuzitoa hizo dead bodies"
Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kujua kila kitakachokuwa kinajiri kuhusiana na tukio hili lililotokea Bunju,Nje kidogo ya jiji la Da es Salaam.
0 comments:
Post a Comment