Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yameshutumu kukamatwa na kushtakiwa kwa waandishi na wanablogu tisa nchini Ethiopia.
Tume ya Kuwalinda Waandhisi wa habari CPJ,
imekosoa serikali ya Ethiopia kwa kutumia sheria ya kukabiliana na
ugaidi, kukandamiza harakati zozote za upinzani nchini humo.Mwandishi mmoja anasema kuwa baada ya wanablogu hao kuzuiliwa na polisi kwa zaidi ya miezi miwili na kufikishwa mahakamani mara kadhaa, hatimaye wameshtakiwa na ugaidi.
Tisa hao sasa wanajulikana kama Zone 9 Bloggers.
Viongozi wa mashitaka wamewashutumu wanabulogu hao sita na wanahabari watatu kwa kupokea ufadhili na maagizo kutoka makundi ya kigaidi yanayolenga kuipindua serikali.
Lakini makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamesema mashitaka hayo ni mojawapo ya mbinu za serikali kuzima upinzani na kukandamiza uhuru wa habari.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn awali ameonya kuwa serikali yake haitasita kupambana na yeyote atakayeonekana kuwa na ushirikiano na makundi yaliyopigwa marufuku nchini humo.
Mara kwa mara Ethiopia imeshutumiwa kwa kuwafunga gerezani waandishi wa habari, wanaoonekana kupinga serikali. Wengine wengi wametoroka nchini humo, wakihofia kukamatwa na kuteswa wakiwa jela.
0 comments:
Post a Comment