Huku harakati za kutaka matumizi
ya Bangi kuhalalishwa zikishika kasi katika sehemu mbali mbali duniani,
Tanzania haijaachwa nyuma.
Wanakijiji katika wilaya ya Makete , mkoa wa
Njombe Kusini Magharibi mwa Tanzania wanataka serikali iweke sheria
ambayo itaweza kuhalalisha matumizi ya mmea huo.Mwenyeketi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Daniel Okoka amesema matumizi ya Bangi katika wilaya hiyo hayajaanza leo, tangu zamani watu kitamaduni walikuwa wakitumia Mbegu za Bangi kukaanga na chakula.
Na kama mmea huo ungekuwa na tahri kubwa kiafya, basi watu wengi wilayani humo wangekuwa vichaa.
Lakini kwa sababu ya sheria kali, matumizi ya Bangi au Marijuana yanafanywa kichinichini katika wilaya hiyo.
0 comments:
Post a Comment