Saturday, 23 August 2014
Atletico Madrid yaichapa Real Madrid na kutwaa Ubingwa wa SUPERCOPA de ESPANA:
Wakicheza katika uwanja wao Estadio Vicente Calderon Atletico Madrid wameifunga Real Madrid goli 1-0 kwenye Mechi ya Marudiano ya Supercopa de Espana na kutwaa Kombe hilo kwa Jumla ya magoli 2-1.
Goli la ushindi kwenye Mechi hii ambayo hubatizwa ‘EL DERBI MADRILEÑO’ lilifungwa katika dakika ya Pili tu ya mchezo na Mchezaji mpya aliyesajiliwa kutokakwa mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munchen Mario Mandzukic likiwa ni goli lake la
kwanza.
Kwenye Mechi ya kwanza kati ya Timu hizo iliyochezwa Jumanne iliyopita na kwenda Sare 1-1 huko El Estadio Santiago Bernabeu.
Jana, Kocha wa Atletico, Diego Simeone, alitolewa nje ya Uwanja na refa baada ya kukwaruzana na Refa wa Akiba.
Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo,hakuanza Mechi hii bali aliingizwa Kipindi cha Pili lakini hakung’ara na Real kujikuta wakimaliza Mtu 10 baada ya Luka Modric kupewa Kadi
Nyekundu.
Wikendi hi Ligi ya Spain, La Liga, itaanza rasmi Jumamosi lakini
Real na Atletico wao wataanza Ligi Jumatatu.
VIKOSI:
Atletico Madrid (Mfumo: 4-2-3-1):
Miguel Angel Moya; Guilherme Siqueira, Miranda, Diego
Godin, Juanfran; Tiago, Gabi; Koke, Raul Garcia,
Antoine Griezmann; Mario Mandzukic
Real Madrid (Mfumoo 4-3-3):
Iker Casillas;Fabio Coentrao, Raphael Varane, Sergio Ramos,
Dani Carvajal; Luka Modric, Xabi Alonso, Toni
Kroos; James Rodriguez, Karim Benzema, Gareth
Bale
0 comments:
Post a Comment