Hospitali moja nchini Marekani
imewaruhusu wamisionary wawili wa kimarekani ambao walikua wakipata tiba
kutokana na kuathiriwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola, na
imethibitishwa hawana athari kwa afya ya jamii.
Dr Kent Brantly na mtabibu mwenziwe Nancy
Writebol ambao waliruhusiwa mapema wiki hii walipata maambukizi ya
ugonjwa huo wakati wakiwasaidia wagonjwa wa ugonjwa huo nchini Liberia.Kufuatia matokeo mazuri ya dawa hiyo ya majaribio dokta huyo wa zamu alijinasibu kuwa kituo chake kimejifunza namna bora ya kumsaidia mgonjwa wa bola na mazingira alimokuwamo, na kuahidi kushirikisha utaalamu huo kwa watabibu kutoka katika nchi za Kiafrica.
Nalo shirika la afya ulimwenguni W.H.O linaandaa mkutano utakao fanyika mwanzoni mwa mwezi huu katika mji wa Geneva nchini uswiss, utakaoangazia namna ya kukabiliana na ugonjwa huu.
Takwimu za hivi karibuni zaonesha kwamba zaidi ya watu elfu kumi na tatu wamekufa kwa ugonjwa huo hasa kutoka katika nchi za Africa Magharibi Liberia,Sierra Leone na Guinea.
0 comments:
Post a Comment