Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, jana,
Alhamisi, Agosti 21, 2014, ameweka historia
nyingine katika ziara yake ya Mkoa wa
Morogoro wakati aliposafiri kwa treni ya
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(TAZARA), ikiwa ni mara yake ya kwanza
kutumia usafiri huo katika kipindi chake cha
Urais.
Rais Kikwete, akifuatana na Mama Salma
Kikwete, amesafiri kilomita 143 ndani ya
Behewa la Kirais (Presidential Coach) la T-
One kwa kiasi cha saa tatu na dakika 25
akitokea stesheni ya Ifakara katika Wilaya ya
Kilombero kwenda Stesheni ya Kisaki, Wilaya
ya Morogoro.
0 comments:
Post a Comment