Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Wednesday, 31 December 2014

BantuTz MAGAZETINI:-SOMA KILICHOANDIKWA KATIKA MAGAZETI YOTE YA LEO DESEMBA 31

 .
BantuTz MAGAZETINI:Ni miongoni mwa huduma bora kabisa tunazozitoa ili wewe mdau wa Bantu usipitwe na habari,stori au taarifa yoyote ile.Tunakuletea kila tunachokipata kwa wakati na muda muafaka.Soma kilichoandikwa katika kurasa za mbele na nyuma magazeti yote ya leo.
 .
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
. Endelea kufurahia huduma za BantuTz.com huku ukiusubiria kwa hamu Mtandao wa kijamii mkubwa na wa kisasa zaidi uitwao Bantuz hapo mwakani.

Monday, 29 December 2014

Korea Kazkazini yamtukana Obama

 
Korea kaskazini imeilaumu Marekani kutokana na mataizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita.
Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananishi rais wa marekani Barack obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa ka filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview
 
Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un.
Korea kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.

Aliyetaka kumuua Papa John Paul amuenzi

 
Mwanamme mmoja raia wa Uturuki aliyempiga risasi na nusura amuue aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki papa John Paul wa pili mwaka 1981 ameweka maua kwenye kaburi lake katika makao makuu ya kanisa katoliki ya Vatican.

Ziara ya Mehmet Ali Agca kwenye makao ya Vatican inafanyika miaka 30 tangu John Paul amtembelee gerezani na kumsamehe kwa kujaribu kumuua.
Bwana Agca aliomba kukutana na kiongozi wa sasa wa kanisa katoliki papa Francis lakini hata hivyo ombi lake lilikataliwa

Aliachiliwa kutoka gerezani nchini Italia mwaka 2000 na kisha baadaye akatumikia kifungo chengine cha miaka 10 nchini Uturuki kwa makosa tofauti.
Hadi sasa sababu zake za kutaka kumuua papa John Paul hazijulikani.

Upepo wakwamisha Uokoaji Meli iliyozama

 
Waokoaji wamekuwa wakipambana na upepo mkali pamoja na mawimbi ya bahari gizani kuwakoa karibu abiria 300 ambao wamekwama ndani ya ferry moja ya Italia iliyokuwa imeshika moto kwenye bahari ya Adriatic.
Maofisa nchini Italia wanasema kuwa oparesheni ya uokoaji itandelea.Hadi sasa watu 190 wamekolewa kutoka kwa ferry hiyo

Shindano la Miss Tanzania lafungwiwa

 
Serikali ya Tanzania imeyafungia kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni.
Mashindano hayo yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na upendeleo mbali na rushwa kulingana na malalamishi yaliotolewa na wananchi pamoja na washiriki.

Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata , Godfrey Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.
Alisema bwana Mgereza:"Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili, lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika mapema mwezi huu, bali kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si kimoja, ni uamuzi mgumu ambao umekuja kutokana na sababu maalumu,"

Imedaiwa kuwa mashindano yaliyofanyika Desemba 12, mwaka huu hayakufikia uamuzi, bali vikao mbalimbali vilivyoendeshwa na wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Basata ndivyo vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa waandaalizi kujipanga upya.
Baadhi ya maswala yaliobainika ni kwamba baadhi ya warembo walidaiwa kutumiwa kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili warembo hao uliofuatwa kuanzia vitongojini hadi kufikia fainali.

Mngereza alisema baraza limegundua kuwa baadhi ya washiriki walichaguliwa kwa upendeleo bila ya kuwa na sifa zilizohitajika

Roboti zapata ajira mgahawani China

 
Mgahawa mmoja nchini China umeanza kutumia Roboti badala ya kuwaajiri hadimu au wafanyakazi wa hotelini kuwapakulia chakula na vinywaji wageni. Hebu tazama mambo yalivyo

Yule gwiji katika uandishi wa vitabu na mtaalamu wa fasihi,Ngugi wa Thiong'o atunukiwa shahada ya udaktari Ujerumani













Ngugi wa Thiong’o ametunukiwa shahada ya Udaktari
wa heshima na Chuo Kikuu cha Bayreuth cha
Ujerumani, huku vitabu vyake “Shetani Msalabani” na
“Matigari” vikiwa vimempatia umashuhuri na
mashaka pia nchini mwake.

Hakuna anaetunukiwa tuzo ya udaktari wa heshma
bila ya kuistahiki. Na Ngugi wa Thiong’o,mwandishi
vitabu na mtaalam wa fasihi amefanya mengi
yanayostahiki tuzo hiyo.Kitabu chake
kilichochapishwa mwaka 1964 kwa kiingereza “Weep
Not,Child” au kwa kiswahili “Usilie mtoto” kilikuwa
kitabu cha kwanza kuchapishwa kwa Kiingereza na
mwandishi vitabu kutoka Afrika Mashariki.
Ngugi wa Thiong’o amesomea katika chuo kikuu
maarufu cha Uganda,Makerere, na pia mjini Leeds
nchini Uingereza.

Baadae aliamua lakini kuandika vitabu vyake kwa
lugha yake ya mama tu,”kikikuyu”.Sababu za
kutafakari lugha gani itumike ameitaja Ngugi wa
Thiong’o katika mahojiano na DW alipoelezea uamuzi
wa kuandika mchezo wa kuigiza pamoja na mtunzi
mwenzake katika mwaka 1976,Ngugi wa Mirii,na
kusema: “Pekee ukweli kwamba tulibidi kujiuliza
michezo ya kuigiza tuiandike kwa lugha gani,inatoa
picha ya jinsi tulivyogeuka kuwa wageni katika nchi
yetu wenyewe kwasababu suala hapo lilikuwa dhahir
nalo ni kwamba tuandike lugha inayozungumzwa na
walio wengi.”
Lugha ya kikikuyu inazungumzwa na zaidi ya watu
milioni sita nchini Kenya na ndio lugha ya mama ya
Ngugi wa Thiong’o na mtunzi mwenzake Ngugi wa
Mirii.

Ngugi wa Thiong’o ameshawahi kufungwa
Kitabu cha mchezo wa kuigiza kilichopewa jina
“Ngaahika Ndeenda” au kwa kiswahili “Nitaowa
wakati nnaotaka” ingawa kilimpatia umashuhuri
mkubwa lakini pia kilimpatia mashaka kutoka
serikalini.Kitabu hicho kilipigwa marufuku na
mwenyewe Ngugi wa Thiong’o kuwekwa korokoroni
kwa muda wa mwaka mmoja.
Lakini kifungo hicho kilimzidishia nguvu za
kuendelea kuandika kwa lugha ya kikikuyu.Huko
huko jela aliandika kitabu chengine akitumia karatasi
za chooni.

Ngugi wa Thiong’o ameshawahi kutunikiwa vyeo
kadhaa vya udaktari wa heshima.
Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha zaidi ya 40.
Katika hati ya kupatiwa shahada hiyo ya udaktari wa
heshima,chuo kikuu cha Bayreuth kinasifu” mchango
wake mkubwa unaostahiki kusifiwa wa kueneza
fasihi ya kiafrika na hasa fasihi kwa lugha za
kiafrika.”Vitabu vyake ni msingi wa matumaini ya
mageuzi katika uhusiano kati ya Afrika na sehemu
nyengine za dunia”-imeandikwa ndani ya hati ya
shahada ya udaktari wa heshima ya chuo kikuu cha
Bayreuth kwa Ngugi wa Thiong’o.


Ndege iliyopotea yaendelea kutafutwa

 
Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.

Chris Brown Na Karrueche Tran Wamerudia rasmi.

chris-brown-and-karrueche-sunofhollywood-4
Hivi karibuni wapenzi Chris Brown na Karrueche Tran wameteka vichwa vya habari kwa kugombana kwenye mitandao na kurushiana vijembe kuhusu mapungufu ya uhusiano wao na nani anasababisha.
Jipya kuhusu hawa ndege wawili ni kwamba walikutana kwenye mkesha wa Krismass na kuongea machache kuhusu mahusiano yao na baadae kukubali kukutana tena.
Watu wa karubi ni Chris wanasema amekuwa akijaribu kurudiana na kumuomba msamaha mpenzi wake Karrueche bila kufanikiwa kwani Tran alikuwa na hasira kila mara akimfikiria Chris.
Maongezi ya mwisho waliyofanya Chris Brown na Karrueche yalikuwa siku ya alhamisi walipokutana kwenye pati ya Chrismass ya Sean Kingston na inasemekana waliondoka pamoja baada ya pati kuisha. Hizi picha zinawaonyesha pamoja.
453-480w 459-480w 464-480w 468-480w

Filamu ya Interview yatikisa mitandaoni

 

Kampuni ya Sony Picutues inasema kuwa - the interview - ambayo ni filamu yenye utata ya dhihaka kuhusu njama ya kumuua kiongozi wa korea kasakzini Kim Jong un imekuwa yenye mafanikio zaidi mtandaoni.
Kampuni hiyo inasema kuwa filamu hiyo imenunuliwa na pia kukodishwa zaidi ya mara milioni mbili kwa muda wa siku nne tangu iwekwe kwenye mitandao.
Sony iliahirisha mpango wake wa filamu baada ya komputa za kampuni hiyo kudaiwa kuingiliwa na wadukuzi,huku Korea Kaskazini ikihusishwa katika udukuzi huo.

Vigogo wa Ligi England waambulia sare

Vigogo Manchester City,Chelsea na Man United wamejikuta wakiambaulia sare katika michezo yao ya ligi ya England.
Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Manchester City waliambulia sare baada ya kuruhusu timu ya Burnley kurudisha mabao mawili yaliyofungwa kipindi cha kwanza na mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2.
Huku vinara wa ligi hiyo Chelsea wakipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Southampton. Sadio Mane aliipa Southampton Bao la kuongoza kabla ya Eden Hazard kuisawazisha timu yake Sekunde chache kabla ya mapumziko.
Manchester United wakiwa ugenini kwenye uwanja wa White Hart Lane walishindwa kutamba mbele ya Tottenham kwa kukubali kutoka sare ya 0-0.

Matokeao ya michezo mingine
Aston Villa 0 - 0 Sunderland
Hull City 0 - 1 Leicester City
Queens Park Rangers 0 - 0 Crystal Palace
Stoke City 2 - 0 West Bromwich Albion
West Ham United 1 - 2 Arsenal
Newcastle United 3 - 2 Everton

Matokeo haya bado yanawabakisha Chelsea kileleni mwa Ligi mbele ya Timu ya Pili Mabingwa Watetezi Man City wakifuatiwa na Man United waliuoko nafasi ya tatu.