Facebook

Sunday, 7 December 2014

"UKIIJUA VIZURI ARSENAL YA WENGER WALA HAIKUPI TABU"


Ukiijua Vizuri Arsenal ya Wenger,!! Wala Hupati
tabu.

Kuna muda utafika itabidi uwaze mambo ya
baadae kwa kuijenga kesho yako.Lakini muda
huo huo wakati Unawaza inabidi usijaribu na
kutoingiza fikra kuwaza vitu ambavyo vipo juu
ya uwezo wako.

Kama Uwezo wako ni wakula
Mchicha kila siku fanya hivyo,Ukitaka Nyama
halafu uwezo wa Kununua nyama Huna utaumia
kwa Hisia kali mnoo.

Wakati Chelsea wanatoa Pesa mfukoni kwa
Roman Abrahimovic walikuwa na malengo yao
kabambe.Walimtwaa Fabregas kwa Paun milion
28, Wakakunjuka tena kwa Diego Costa Pauni milion
30.

Yote hayo wanayafanya kwa
malengo.Malengo ambayo Manchester City na Manchester United huwa
wanayalenga.Tena unapoona timu inapambana
Dakika zote kutafuta Pointi 3 kwa Jasho ujue
kuna kitu wanakitafuta.Kuna Kitu ndani ya Akili
yao kipo.

Wanawaza Ubingwa,Ndo maana Chelsea
ya msimu uliopita ilikosa Ubingwa kwa Sababu ya washambuliaji wabovu wasio na malengo walio kuawa nao.Wakaa chini wakaona Ni
vyema Wamlete Remy,Wamlete Costa na kurudisha hadhi ya timu na kuongeza morali kwa kumleta kumrudisha mtu anayeijua Chelsea nje ndani Drogba,kisha wakamleta
Fabregas aje kuwapikia mabao.

Manchester City ya msimu ukiopita ilikuwa inaparangana dakika
zote.Unapomuona Aguero akizunguka  na Mpira ni
wazi unaona Kuna kitu kajengwa kwenye akili
yake.Unapomtazama Yaya Toure dhahiri shahiri unaona
hachezi ili mradi,bali anacheza kwa malengo
flani,anakimbia uku na kule kuhakikisha zinapatikana Pointi tatu.

Hivyo vivyo kwa
Kompany anavyokaba,anakaba mpaka unajiuliza
timu ya baba yake ama ana hisa apo?

Lakini hapana,ni malengo yaliyo katika akili zake ya kuwa
hapa tunacheza kwa Kuutafuta Ubingwa na si vinginevyo.

Arsene Wenger na timu yake,wachezaji wake,mpaka
mashabiki wake hakuna mwenye malengo ya
Ubingwa.Chelsea ikiwaza Ubingwa akili yako
haitapinga,City ikiwaza ubingwa akili yako
itakubali,Manchester United wakiwaza ubingwa huwa inajionyesha wazi,kipindi cha Sir Alex Ferguson alikuwa na majira maalum ya kukutabiria ubingwa,alikuwa anasema ikifika Chrismas anaongoza Ligi ubingwa ni wake nadhani hata kisaikolojia ilikuwa inawajenga wachezaji.

Lakini Arsenal hii kuwaza Ubingwa
mkubwa wa EPL  ama UEFA ni Upuuzi.Nadhani ata akili yako itakataa japo mdomo utanena.

Arsene Wenger kawajenga wachezaji kwa kucheza mechi ya leo vizuri ili Kesho awe kikosi cha kwanza.Wachezaji nao washajijengea Watacheza vizuri kwa uwezo wa hali ya Juu mnoo ili waitwe timu za taifa.

Hakuna mchezaj ambaye unamuona anawaza Ubingwa.Sio wa leo wala wa jana.Sio wajuzi ama
wa mtondogoo.Sote tunajua Ubingwa wetu upo
nafasi nne za juu ndio maana Leo tutakaza ilo tufikie
malengo yetu.Malengo ya kuingia nafasi nne za juu ambayo ndiyo
Ubingwa wetu wa kila siku.

Unashangaa Koscienly kuwekwa benchi wakati
hana.Majeraha yoyote?
Usishangae! apa hakuna
tunachokitafuta zaidi ya nafasi nne za juu tucheze UEFA.

Unataka Ushindi Unampanga Belletin kulia wakati
Chambers yupo fiti huo si Upuuzi?
Leo timu inafuzu kucheza Ligi ya mabingwa ulaya.

Timu itasogea hatua Mbili mbele halafu inatolewa kwenye hatua ya 16 bora na tukijikaza sana labda
robo fainali.Kwa nini kila siku timu inaishia hatua ya Robo fainali au 16 bora?

Kwa nini kila msimu timu inamaliza nafasi nne za juu hata nafas
ya 3 hatugusi? Kwa miaka ya hivi karibuni.

Hayo Ndo malengo ya Arsene Wenger.Ndo maana hushtuki timu kucheza hovyo kipindi cha kwanza
sababu malengo ya timu tunayajua.

Na ukiangalia
kwa makini timu inacheza bila mipango.Usajili
Bila Mipango.Timu inacheza kudhihirisha kutaka
Ubingwa wa nafasi ya nne na ubingwa wa Ligi au wa UEFA.

Jana Arsenal ilikuwa na Makosa ya mipira mifupi,Kesho kocha
anasema timu ni mbovu kwenye krosi, kesho
nako atasema timu ni mbovu kwenye mipira ya
juu.

Huyu kocha kosa analiona na hataki
kulifanyia kazi,Dhahiri Arsenal inacheza kukamilisha
ratiba,haipo kiushindani.

Ukiyajua matatizo ya arsene hutaumia
sana,ukishayajua malengo ya Arsene Wenger kila siku
hitauwaza Ubingwa,hutajipa presha wala Kujipa
ma-stress.

Nitahuzunika Asenal ikikosa nafasi ya nne na ninaamini ni funyu sana nazipa nafasi Chelsea,Manchestet City na Manchestet United,hiyo ya nne itategemea atakayekaa vizuri kati ya Arsenal,Southampton,Liverpool,Tottenham n.k

Nitahuzunika ikishindwa kufuzu
hatua ya makundi.Lakin sitahuzunika Arsenal ikiukosa ubingwa.

Endelea kutembelea www.bantutz.com kwa mbalimbali za kuvutia.

Imeandaliwa na............

Katemi "Mugisha" Methsela"

0 comments:

Post a Comment