Manchester United inaweza kutumia mpaka
kiasi cha pauni milioni 350 kwa kipindi cha
miaka miwili katika kusajili wachezaji
wapya.
Hii inaweza kufikiwa kama watafanikiwa
kuwasajili kiungo Kevin Strootman 24,toka
roma, na beki wa Borussia Dortmund Mart
Hummels, 25,pia inasadikika kocha Louis van
Gaal anamtaka beki wa kulia wa Southampton
Nathaniel Clyne, 23.
Arsenal wako tayari kurekebisha safu yao ya
kiungo kwa kumuwania kiungo Morgan
Schneiderlin, toka Southampton kwa dau la
pauni milioni 15 pia wako tayari kutoa pauni
milioni 8 kwa beki Tyrone Mings, 21,wa
Ipswich Town.
Inter Milan wanaangalia uwezekano wa
kumsajili mshambulaiji Joel Campbell, wa
Arsenal raia wa Costa Rica pamoja na kiungo
wa Tottenham Erik Lamela 22.
Henrique Pompeu wakala wa mshambuliaji wa
Colombia Jackson Martinez 28, ameeleza kuwa
mteja wake huyo hato ondoka katika timu yake
ya Fc Porto japo timu za Arsenal, Liverpool na
Tottenham zimekua zikimuwania.
Meneja wa Newcastle Alan Pardew,
anawasiwasi nyota wake Moussa
Sissoko,ataondoka St James' Park kuelekea
Arsenal katika usajili wa dirisha dogo mwezi
januari.
Real Madrid na Paris St-Germain wanapigana
vikumbo kuweza kupata saini ya mshambuliaji
Eden Hazard.Huku chelsea wakiwa tayari
kumboreshea kandarasi yake ya sasa nyota
huyo wa ubelgiji mwenye miaka 23.
Kiungo wa kibrazil Luca Silva,21,anayechezea
klabu ya Cruzeiro yuko tayari kuzikata ofa za
Manchester United na Arsenal ili kujiunga na
miamba wa hispania Real Madrid.
Timu Leicester City itajaribu kutaka kumrejesha
tena kwenye ligi ya Epl mshambuliaji Jermain
Defoe, 32,toka klabu ya Toronto Fc.
0 comments:
Post a Comment